• HABARI MPYA

    Wednesday, June 18, 2014

    BALOTELLI SASA KARIBU KUTUA ARSENAL, WAKALA WAKE ASEMA GUNNERS NI KLABU NZURI

    MSHAMBULIAJI Mario Balotelli sasa milango iko wazi kutua Arsenal baada ya wakala wake kusema kwamba 'chochote kinawezekana' katka dirisha hili la usajili.
    Mpachika mabao huyo wa Italia, aliyefunga bao la ushindi dhidi ya England katika Kombe la Dunia Jumamosi iliyopita, yumo kwenye orodha ya wachezaji wanatakiwa na kocha Arsene Wenger.
    Arsenal imewasiliana na wakala wake, Mino Raiola katika harakati za kutaka kumng'oa mshambuliaji huyo AC Milan na wakala huyo hajakataa.
    Anaweza kuhamia Emirates: Wakuu wa Arsenal wanaamini wanaweza kumpata Balotelli katakana na AC Milan kutaka kupunguza bajeti yao ya mishahara
    "Arsenal ni klabu nzuri,"amesema wakala wa Balotelli, Mino Raiola akihojiwa na Sky Sports. "Atahamishwa? Chochote kinawezekana,".
    Arsenal intake kwanza kujua gharama za kumsajili Balotelli kabla ya kuanza jitihada rasmi za kumnunua. AC Milan iko tayari kumtoa mchezaji huyo mtata, kwa sababu wanataka kupunguza bajeti yao ya mishahara msimu ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BALOTELLI SASA KARIBU KUTUA ARSENAL, WAKALA WAKE ASEMA GUNNERS NI KLABU NZURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top