• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 23, 2014

  STRAIKA MPYA AZAM FC DIARA ASEMA; “NITANG’ARA BONGO”

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI mpya wa Azam FC kutoka Mali, Ismaila Diara amesema kwamba atajihitaji muda kuzoea mazingira ya soka ya Tanzania kabla ya kuanza kuwika.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam mchezaji huyo mwenye mwili mkubwa amesema kwamba hajui lolote kuhusu soka ya Tanzania na yote atajifunza hapa. 
  Ismaila Diara amesema anaamini atang'ara katika soka ya Tanzania baada ya kuzoea mazingira

  “Sijui, sijui kabisa, mimi ni mchezaji na naweza kucheza popote. Nitahitaji muda kidogo nizoee, ila nina amini nitafanya vizuri,”amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STRAIKA MPYA AZAM FC DIARA ASEMA; “NITANG’ARA BONGO” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top