• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 25, 2014

  KAMPENI ZAANZA SIMBA SC, KILA MTU AAHIDI MAMBO MATAMU MSIMBAZI

  Na Nagma Said, DAR ES SALAAM
  WAGOMBEA wanaowania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Simba unatakaofanyika June 29 wamepigana vikumbo kwenye kampeni zilizozinduliwa juzi baada ya kila mmoja kuamua kunadi sera zake.
  Wagombea hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakianisha sera zao ili wanachama wa klabu hiyo wawape nafasi ya kuwachagua.
  Mgombea, Evans Aveva jana amejitokeza rasmi kwa kuzindua kampeni zake katika hotel iliyopo kwenye jengo la Raha Tower Dar es Saalam.
  Evans Aveva anagombea Urais wa Simba SC

  Evans aliyesindikizwa na Mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Hassan Dalali amesema akifanikiwa kuingia madarakani kitu atakachoanza nacho ni kujenga umoja na kuondoa makundi kwenye klabu hiyo.
  Eveva aliyeanza kuongoza  Simba toka mwaka 1993 alisema mbali na umoja sera ya pili ni kucheza mpira na kufanikiwa kulinda heshima yao.
  “Huu ni mwaka wa tatu Simba tumekuwa hatushiriki mashindano yoyote hivyo nikipewa ridhaa nitaanza naandaa timu za Under 17, 20 na zaidi ili kuisaidia Simba kutwaa Ubingwa,”alisema.
  Aveva ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Usajili alisema iwapo atafanikiwa kuingia madarakani kocha wao Logarusic ataendelea kuinowa timu hiyo mpaka watakapojipanga.
  “Ligi inaanza Septemba na sisi kama tukifanikiwa kuingia madarakani tutakuwa na muda mchache hivyo hatuwezi kumuondoa Logarusic mpaka  tutakapojipanga,”alisema
  Alisema mbali na kutomuondoa Logarusic wanatarajia kuwasomesha wachezaji wa zamani wa timu hiyo ili wapate walimu wazuri watakaokuwa na Simba.
  “Tunataka kuwa na walimu wetu wenyewe, wapo wengi ambao walishaitumikia Simba hivyo tutawaboresha ili kupunguza gharama,”alisema.
  Aveva naye anayeungwa mkono na tawi la Friend of Simba, aliwataka wanachama wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kwani uzoefu alionao atahakikisha anafanya usajili ‘bob kubwa’.
  “Nina uzoefu wa suala nzima la usajili kwa kipindi cha miaka 10, hivyo tutasajili kikosi bora kitakachosaidia kutupa ubingwa msimu huu hivyo wanachama wasiwe na wasiwasi,”alisema.
  Nae mgombea wa nafasi ya makamu wa Rais, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ alisema watahakikisha wanasajili vifaa imara ili mashabiki wao waweze kumsahau winga Emanuel Okwi aliyesajiliwa na Yanga.
  Wakati Kaburu akiyasema hayo, Swed Mkwabi anayewania nafasi hiyo hiyo ameibuka na sera ya pointi tatu.
  Uchaguzi wa Simba umepangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu licha ya uchaguzi huo kutinga mahakamani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAMPENI ZAANZA SIMBA SC, KILA MTU AAHIDI MAMBO MATAMU MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top