• HABARI MPYA

    Tuesday, June 24, 2014

    NYOTA WA KWANZA KUSAJILIWA NA VAN GAAL MAN UNITED AWEZA KUWA HUYU HAPA

    KIUNGO Ander Herrera anakaribia kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Manchester United ya England, Louis van Gaal kwa dau la Pauni Milioni 28.4.
    Mchezaji huyo wa Athletico Bilbao amekuwa akitakiwa na klabu hiyo ya Ligi Kuu England tangu msimu uliopita, lakini sasa kocha mpya wa Mashetani hao Wekundu, Van Gaal has anaelekea kufanya kweli kumnasa nyota huyo.
    Anakuja: Ander Herrera anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Louis van Gaal Manchester United kwa Pauni Milioni 28.4

    WASIFU WA ANDER HERRERA

    Kuzaliwa: Bilbao, Hispania, Agosti 14 1989 (Miaka 24)
    USHIRIKI WA LIGI
    2008-2009: Zaragoza B (mechi 10, mabao 2)
    2009-2011: Zaragoza (mechi 82, mabao 6)
    2011- HADI SASA: Athletico Bilbao (mechi 94, mabao 7)
    TIMU ZA TAIFA
    2009-2009: Hispania U20 (mechi 10, mabao 3)
    2009-2011: Hispania U21 (mechi 15, mabao 4)
    2012-HADI SASA: Hispania U23 (mechi 5, hajafunga bao)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NYOTA WA KWANZA KUSAJILIWA NA VAN GAAL MAN UNITED AWEZA KUWA HUYU HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top