• HABARI MPYA

    Wednesday, June 25, 2014

    IVORY COAST NAYO NJE, COLOMBIA NA UGIRIKI ZAUFU KUNDI C KOMBE LA DUNIA

    IVORY Coast imekuwa timu ya pili ya Afrika kuaga mapema Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa mabao 2-1 na Ugiriki usiku huukatika mchezo wa mwisho wa Kundi C.
    Mabao yaliyowazamisha Ivory Coast usiku huu yamefungwa na Giorgios Samaras dakika ya 42 na Samaras  90 na ushei kwa penalti.
    Giorgios Samaras akishangilia baada ya kuifungia Ugiriki

    Wilfried Bony aliifungia bao pekee Ivory Coast dakika ya 74 katika mchezo ambao timu hiyo ilihitaji sare kwenda 16 Bora. Colombia imemaliza na ushindi wa 4-1 dhidi ya Japan na kufikisha pointi tisa, mbele ya Ugiriki yenye pointi nne, Ivory Cpast poiniti tatu na Japan pointi moja.
    Kikosi cha Ugiriki kilikuwa; Ugiriki, Karnezis/Glykos dk26, Maniatis, Manolas, Samaras, Kone/Samaris dk11, Karagounis/Gekas dk24, Salpingidis, Torosidis, Lazaros, Sokratis na Cholevas.
    Ivory Coast; Barry, Boka, Kolo Toure, Bamba, Serey 6; Kalou 6, Tiote/Bony dk61, Gervinho/Sio, dk83, Drogba/Diomande dk78, Aurier na Yaya Toure.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IVORY COAST NAYO NJE, COLOMBIA NA UGIRIKI ZAUFU KUNDI C KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top