• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 28, 2014

  KABURU: NINATAKA KUIRUDISHA SIMBA SC NJIA KUU, IMECHEPUKA

  Na Samira Said, DAR ES SALAAM
  MGOMBEA wa nafasi ya Makamu wa Rais, Geofrey Nyange' Kaburu' amewaambia wanachama wa Simba wamchague ili Simba irudi njia kuu.
  Njia kuu Kaburu aliielezea ni ushindi na si kukaa mchepuko sehemu ambayo Simba haistahili kuwepo.
  Kaburu alisema pia yeye kamwe hagawi wachezaji kama inavyoelezwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.
  Alisema kila timu inapokwama yeye hutafutwa na kuokoa jahazi.
  Kaburu anataka kuirudisha Simba SC njia kuu

  Alisema akifanikiwa kuingia madarakani yeye na mgombea Urais, Evans Aveva, watailetea Simba ushindi na pointi tatu.
  Alisema pia hauzi wachezaji  bali kamati ya utendaji ndiyo huuza wachezaji kwa kufanya makubaliano kihalali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KABURU: NINATAKA KUIRUDISHA SIMBA SC NJIA KUU, IMECHEPUKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top