• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 23, 2014

  UHOLANZI YAIPIGA CHILE 2-0, HISPANIA YAAMBULIA USHINDI KOMBE LA DUNIA

  ASILIMIA 100. Naam, Uholanzi imefuzu kuingia 16 Bora ya Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kushinda mechi zake zote za Kundi B, ikimaliza na ushindi wa mabao 2-0 leo dhidi ya Chile.
  Mabao ya Fer dakika ya 77 na Depay dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutiku dakika 90 za kawaida, yanifanya ‘Chungwa’ imalize na pointi tisa mbele ya Chile yenye pointi sita inayofuzu pia.
  Arjen Robben akiwatoka mabeki wa Chile
  Waliokuwa mabingwa watetezi, Hispania wameambulia pointi tatu baada ya kufunga 3-0, Australia leo inayomaliza bila pointi hata moja.
  Mabao ya Hispania yamefungwa na David Villa dakika ya 36, Fernando Torres dakika ya 69 na Juan Mata dakika ya 82
  Kocha Vicente del Bosque leo aliwapanga Reina, Juanfran, Ramos, Albiol, Alba, Cazorla aliyempisha Fabregas dakika ya 68, Alonso aliyempisha Silva dakika ya 83, Koke, Iniesta, Torres na Villa aliyempisha Mata dakika ya 57.Something to cheer: Fernando Torres celebrates his goal
  Angalau: Fernando Torres akipongezwa na wenzake baada ya kufunga

  Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen, Blind, Vlaar, De Vrij, Kuyt/Kongolo dk89, De Jong, Wijnaldum, Janmaat, Sneijder/Fer dk75, Lens/Depay dk69 na Robben.
  Chile; Bravo, Silva/Valdivia dk70, Medel, Jara, Isla, Aranguiz, Diaz, Mena, Gutierrez/Beausejour dk46, Vargas/Pinilla dk81 na Alexis.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UHOLANZI YAIPIGA CHILE 2-0, HISPANIA YAAMBULIA USHINDI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top