• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 24, 2014

  CAMEROON YATIA AIBU BRAZIL, NEYMAR AENDELEA KUNG'ARA...MEXICO NAYO YAPETA

  WENYEJI Brazil wamekamilisha mechi za kundi lake, A kwa ushindi wa mabao 4-1 usiku wa kuamkia leo dhidi ya Cameroon Uwanja wa Nacional. 
  Mshambuliaji tegemeo Neymar alifunga mabao mawili dakika za 17 na 34, wakati mabao mengine yalifungwa na Fred dakika ya 49 na Fernandinho dakika ya 84.
  Bao pekee la Simba Wasiofungika wanaoaga michuano hiyo bila hata pointi moja baada ya awali kufungwa pia na Croatia na Mexico, lilifungwa na Matip dakika ya 26.
  Mexico nayo ilimaliza na ushindi wa 3-1 dhidi ya Croatia, mabao yake yakifungwa na Rafael Marquez, Andres Guardado na Javier Hernandez. Bao la kufutia machozi la Croatia iliyompoteza mchezaji wake Ante Rebic aliyetolewa kwa kadi nyekundu mwishoni mwa mchezo, lilifungwa na Ivan Perisic. Brazil inamaliza na pointi saba sawa na Mexico, lakini inakaa kileleni kwa wastani mzuri zaidi wa mabao.
  Nyota: Neymar amefunga mabao mawili dhidi ya  Cameroon
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAMEROON YATIA AIBU BRAZIL, NEYMAR AENDELEA KUNG'ARA...MEXICO NAYO YAPETA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top