• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 25, 2014

  YANGA SC WAANZA ‘MDOGO MDOGO’ UFUKWENI WAKATI KOCHA MAXIMO AWEZA TUA KESHO DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAKATI kocha mpya Mbrazil, Marcio Maximo anatarajiwa kuwasili kesho, kikosi cha Yanga SC kimeanza mazoezi ya ufukweni asubuhi ya leo.
  Wachezaji nane walijitokeza katika mazoezi hayo ya kuanza kujiandaa na msimu mpya kwenye ufukwe wa Cocoa, Dar es Salaam.
  Wachezaji zaidi wanatarajiwa kujitokeza kuanzia kesho, huku klabu hiyo ikiendelea na mchakato wa usajili baada ya kutema wachezaji 11 kutoka kikosi cha msimu uliopita na wawili kuondoka. 

  Yanga imewaacha kipa Yusuph Abdul, mabeki David Luhende, Ibrahim Job, viungo Athuman Idd 'Chuji', Geroge Banda, Rehani Kibingu, Hamisi Thabiti, Bakari Masoud, Abdalllah Mguhi ‘Messi’ na washambuliaji Reliants Lusajo na Shaaban Kondo.
  Kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu wamehamia Azam FC. Lakini tayari Yanga SC imekamilisha usajili wa wawili wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij.
  Wachezaji waliosajiliwa ni beki Pato Ngonyani, kiungo mkabaji, Said Juma na mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Saleh Abdallah. Ngonyani anayecheza kushoto na nafasi zote za kati, amesaini Mkataba wa miaka mitatu, wakati Said Juma amesaini miaka miwili na Saleh Abdallah amesaini miaka mitatu pia.
  Aidha, Yanga SC imewaongezea mikataba wachezaji wake Jerry Tegete, Said Bahanuzi, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Ally Mustafa ‘Barthez’ ambao wote wamesaini miaka miwili kila mmoja.
  Yanga SC imesitisha mpango wa kumtema kiungo Nizar Khalfan ambaye amebakiza mwaka mmoja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WAANZA ‘MDOGO MDOGO’ UFUKWENI WAKATI KOCHA MAXIMO AWEZA TUA KESHO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top