• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 20, 2014

  ITALIA YAANGALIA MLANGO WA KUTOKEA KOMBE LA DUNIA BAADA YA KUPIGWA 1-0 NA COSTA RICA

  MATUMAINI ya England kufuzu 16 Bora ya Kombe la Dunia yameyeyuka baada ya Costa Rica kuifunga Italia 1-0 katika mchezo wa Kundi D Kombe la Dunia. 
  Haya ni matokeo mabaya zaidi kwao tangu mwaka 1958 wakifungwa mechi mbili za mwanzo na Italia na Uruguay, ambao sasa watatoana jasho katika mchezo wa mwisho kuwania kuungana na Costa Rica kutoka kundi hilo kwenda Raundi ya Pili.
  Shujaa; Bryan Ruiz ndiye ameiweka karibu na mlango wa kutokea Italia

  Bao pekee la Bryan Ruiz dakika ya 44 jioni ya leo ndilo limeizamisha Italia, ambayo nayo sasa iko mguu nje, mguu ndani kwenye fainali za mwaka huu.
  England itamaliza na vinara wa kundi hilo, Costa Rica waliozitoa nishai Italia na Uruguay, ikiwa tayari imeaga. 
  Italia: Buffon, Abate, Barzagli, Chiellini, Darmian, Motta/Cassano dk45, Pirlo, De Rossi, Candreva/Insigne dk56, Balotelli na Marchisio/Cerci dk69.
  Costa Rica: Navas, Duarte, Gonzalez, Umana, Gamboa, Borges, Tejeda/Cubero dk67, Diaz, Ruiz/Brenes dk81, Campbell/Urena dk74 na Bolanos.
  So close: Mario Balotelli was sprung clear and beat the goalkeeper but his lob bounced wide
  Mario Balotelli alikosa mabao mawili ya wazi 
  Grounded: Andrea Pirlo did not inspire Italy as he had done against England
  Andrea Pirlo akipambana katikati ya Uwanja
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ITALIA YAANGALIA MLANGO WA KUTOKEA KOMBE LA DUNIA BAADA YA KUPIGWA 1-0 NA COSTA RICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top