• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 30, 2014

  ROBBEN AKIRI KUJIANGUSHA KUMDANGANYA REFA AWAPE PENALTI UHOLANZI

  WINGA Arjen Robben alijaribu kumdanganya refa katika mchezo wa 16 Bora jana Kombe la Dunia, Uholanzi ikiifunga mabao 2-1 Mexico na kwenda Robo Fainali.
  Mholanzi huyo alisema kwamba alijirusha kutafuta penalti, lakini lie iliyotolewa dakika ya tatau ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, ambayo Uholanzi waliitumia kusonga mbele katika mbio za kukimbilia Kombe la Dunia.
  Robben aliomba penalti mbili zilizokjataliwa mapema katika mchezo huo - kabla ya Klaas Jan Huntelaar kufunga dakika za majeruhi bao la ushindi - na baadaye akaomba radhi kwa kujaribu kutaka kumdanganya refa Mreno, Pedro Proenca.

  Hii ilikuwa sahihi: Robben akiruka kwenda chini na refa Mreno, akawapa penalti Uholanzi dakika za majeruhi

  "Lazima niombe radii "amesema Robben. "Moja [mwishoni] ilikuwa penalti, lakini nyingine zile zilikuwa za kujirusha kipindi cha kwanza. Nisingefanya hivyo.'
  Robben alipewa penalti ya dakika za lala salama baada ya kuangushwa na Nahodha wa Mexico, Rafael Marquez, lakini nyota huyo wa Bayern Munich awali alikataliwa matatuta mawili aliyolilia, wakayti timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0.
  Baadaye Uholanzi ikasawazisha, zikiwa zimebaki dakika tatu mchezo kumalizika kupitia kwa Wesley Sneijder na katika dakika za majeruhi, Robben akaangushwa katika penalti iliyokubalika na Huntelaar akaifungia timu hiyo bao la ushindi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ROBBEN AKIRI KUJIANGUSHA KUMDANGANYA REFA AWAPE PENALTI UHOLANZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top