Na Saidy Mdoe, DAR ES SALAAM
HAKUNA mwanamuziki wa Mashujaa Band atakayeshiriki onyesho maalum la Twanga Pepeta litakalojulikana kama Usiku wa Mwana Dar es Salaam.
Akiongea kwa njia ya simu na Saluti5, Mkurugenzi wa Masoko wa wa Mashujaa, Max Luhanga, aliweka wazi juu ya ushiriki wa wasanii wa bendi yao kwenye onyesho hilo la Mwana Dar es Salaam.
Onyesho la Mwana Dar es Salaam litafanyika Jumamosi Juni 21 ndani ya ukumbi wa Mango Garden.
Miongoni mwa wasanii wa Mashujaa Band waliotajwa kushiriki onyesho hilo ni Chaz Baba, Ferguson na Super K.
Sifa kuu ya kushirikishwa kwenye usiku wa Mwana Dar es Salaam ni uwe mmoja kati ya wasanii waliopita Twanga Pepeta na kushiriki katika albam ya Mwana Dar es Salaam iliyotoka mwaka 2009.
Max Luhanga amesema kwa siku hiyo Mashujaa Band watakuwa na onyesho maalum la kukodiwa ambapo moja ya masharti ya mteja wao ni uwepo wa wasanii wote waandamizi.
“Kama tungepewa taarifa mapema kabla hatujaongea na mteja wetu pengine tungekuwa na namna ya kusaidia onyesho hilo la Mwana Dar es Salaam,” anafafanua Max.
“Kwa faida ya wakati ujao, mambo kama haya yanatakiwa yaende kiofisi kabla hayajatangazwa hadharani, tumekuwa tukipata taarifa hizi kupitia vyombo mbali mbali vya habari, lakini sisi kama Mashujaa hatujapata taarifa official.
“Tunawaomba radhi waandaji wa Mwana Dar es Salaam, tunawatakia kila la kheri na tunaamini onyesho lao la Mwana Dar es Salaam litafana,” alimaliza Max Luhunga.

0 comments:
Post a Comment