// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NEYMAR AING’ARISHA BRAZIL KOMBE LA DUNIA, YAICHAPA CROATIA 3-1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NEYMAR AING’ARISHA BRAZIL KOMBE LA DUNIA, YAICHAPA CROATIA 3-1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, June 13, 2014

    NEYMAR AING’ARISHA BRAZIL KOMBE LA DUNIA, YAICHAPA CROATIA 3-1

    Na Nurat Mahmoud, SAO PAULO
    MWANZO mzuri kwa Neymar akifunga mabao mawili usiku huu, wenyeji Brazil wakianza vyema Fainali za Kombe ka Dunia kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Croatia Uwanja wa Corinthias, mjini Sao Paulo.
    Croatia waliotawala sehemu ya kiungo, waliuanza vizuri mchezo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 11.
    Sifa zimuendee Olic aliyepiga krosi nzuri kwa Nikica Jelavic na katika harakati za kuokoa, Marcelo wa Brazil aliutumbukiza mpira kwenye lango lake.
    Mwanzo mzuri; Neymar amefunga mabao mawili Brazil ikishinda 3-1 dhidi ya Croatia usiku huuSpot on (just about): Neymar puts his penalty past Stipe Pletikosa despite the Croatia keeper getting a hand to it
    Neymar akimfunga kwa penalty kipa Stipe Pletikosa wa Croatia aliyekaribia kuokoa mkwaju huo kama si kuupangulia nyavuni kwake

    Croatia waliendelea kutawala mchezo baada ya bao hilo, lakini Brazil waiendelea nao kupambana kusaka bao la kusawazisha.
    Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 29 baada ya Neymar kuisawazishia Brazil kufuatia shambulizi la kushitukiza- baada ya kipa Julio Cesar kuokoa mpira wa kichwa wa Jelavic na kuanzisha shambulizi haraka.
    Brazil ilipata bao la ushindi kwa penalti dakika ya 71 baada ya Fred kujiangusha wakati anakabiliana na Dejan Lovren kwenye eneo la hatari na Neymar akaenda kufunga tena.
    Oscar alihitimisha ushindi wa Brazil kwa bao la tatu dakika ya 90 na ushei na kuwapa faraja mashabiki wa nyumbani.
    Kikosi cha Brazil kilikuwa: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Paulinho/Hernanes dk63, Gustavo, Hulk/Bernard dk68, Oscar, Neymar/Ramires dk88 na Fred.
    Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Lovren, Vrsaljko, Modric, Rakitic, Perisic, Kovacic/Brozovic dk61, Olic na Jelavic/Rebic dk78.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NEYMAR AING’ARISHA BRAZIL KOMBE LA DUNIA, YAICHAPA CROATIA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top