• HABARI MPYA

    Thursday, June 12, 2014

    MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI UTAKAVYOWAATHIRI NYOTA WAISLAMU KOMBE LA DUNIA, UTAANZA SAMBAMBA NA RAUNDI YA PILI

    BAADHI ya nyota wanaotarajiwa kuziongoza timu zao kwenye Kombe la Dunia wanatarajiwa kuwa na wakati mgumu mara utakapoanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
    Hii itakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986 ibada hiyo ya waislamu inakuja wakati wa mashindano hayo ya Kombe la Dunia.
    Waislamu wanafunga kutwa nzima wakati wa Ramadhani na hawaruhusiwi kula wall kunywa wakati huo, hali ambayo itawaathiri wachezaji waumini wa dini hiyo katika Kombe la Dunia.  
    Ramadhani itaanza Juni 28 – siku ya kwanza ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na itakwenda hadi Julia 27 na nchi kama Ufaransa na Ivory Coast zitaathirika zaidi zikiingia Hatua ya 16 Bora, kwani wachezaji wake wengi ni waislamu safi.

    Mtu na kaka yake: Wachezaji wawili ndugu wa Ivory Coast, Yaya (kushoto) na Kolo Toure ni waislamu safi
    Faith: Real Madrid's Karim Benzema is one of France's high-profile Muslim stars
    Muumini safi: Nyota wa Real Madrid, Karim Benzema ni miongoni mea wachezaji Waislamu wa Ufaransa
    Belief: Switzerland forward Xherdan Shaqiri is another European star of Muslim faith
    Mshambuliaji wa Uswisi, Xherdan Shaqiri ni Muislamu pia

    Nyota wa Ufaransa akiwemo mshambuliaji wa Real Madrid’s Karim Benzema, Mamadou Sakho wa Liverpool, beki wa Arsenal, Bacary Sagna na Moussa Sissoko wa Newcastle wote Waislamu.
    Wakati huo huo, Ndugu wawili wa Ivory Coast, Yaya na Kolo Toure – wa Manchester City na Liverpool pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho na kiungo wa Newcastle, Cheick Tiote nao pia ni Waislamu safi.
    Sehemu kubwa ya wachezaji wa Bosnia– akiwemo mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko – ni Waislamu pia, sawa na wachezaji wawili wa Ubelgiji wanaocheza Ligi Kuu ya England, Marouane Fellaini na Moussa Dembele, tegemeo la Uswisi, Xherdan Shaqiri na kiungo Mjerumani wa Arsenal, Mesut Ozil.
    Kitu kimoja kizuri kwa wachezaji hao ni kwamba kwa sasa kutwa moja ina saa 11 mjini Rio de Janeiro, ukilinganisha na saa 17 za Uingereza.
    Baadhi ya wachezaji wa kiislamu huachana na ibada hiyo wakati wa mashindano, lakini winging kama Kolo Toure, wan a msimamo mkali na huendelea kufunga.
    Top man: Germany's Mesut Ozil will be one of his country's key players
    Mtu mkubwa: Nyota wa Ujerumani, Mesut Ozil ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa nchi yake
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI UTAKAVYOWAATHIRI NYOTA WAISLAMU KOMBE LA DUNIA, UTAANZA SAMBAMBA NA RAUNDI YA PILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top