Na Samira Said, DAR ES SALAAM
WANACHAMA wa Simba SC wamesema kwamba kumchagua Michael Richard Wambura kuwa Rais wao ni sawa na kufungua tawi la Yanga SC katika klabu yao, jambo ambalo wanaona ni hatari.
Wakizungumza na BIN ZUBEIRY leo Dar es Salaam, wanachama hao wakiongozwa na Dk Mohammed Wandwi wamesema kwamba Wambura ni mtu ambaye anaungwa mkono na watu wa Yanga SC, wakiongozwa na kigogo wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF).
Wandwi amesema Wambura anabebwa mno na kigogo huyo wa TFF na watu wa Yanga SC, ili afanikiwe kuwa Rais wa Simba SC.
“Wasiwasi wetu ni kwamba, huyu Wambura akishakuwa Rais w Simba SC, Yanga watanufaikaje? Inafahamika sisi na Yanga ni wapinzani, sasa inapokuwa kiongozi wetu mkuu tunachaguliwa na Yanga, inaashiria nini?”alihoji Wandwi.
Kwa upande wake, mwanachama mwingine Ras Simba amewataka wanachama wenzake wa Simba SC kufungua macho na kujihadhari na mkakati unaopangwa na Yanga SC kuweka watu wao kwenye klabu yao.
“Nina wasiwasi sana sisi tutakuwa wa kufungwa hata 10-0 na Yanga, na tusahau kuhusu ubingwa na ninadhani utakuwa mwanzo wa kifo cha Simba, haiwezekani watu wa Yanga watuchagulie sisi kiongozi.
Yaani hata wakati wa sakata lake, wana Yanga ndio waliokuwa wanaongoza kufurahia arejeshwe kugombea, kwa sababu wanajua ni Yanga mwenzao, vikao vyake vya mikakati huwa anakuwa na.......(Rais wa zamani wa Yanga) na ............(kigogo wa TFF) pale Kinondoni. Hawa watu wanasuka mkakati upi mzuri kwa Simba SC?”alihoji mwanachama mwingine, Omary Maslahi.
Naye Said Mohammed ‘Bedui’ amewasihi wanachama wenzake wa Simba SC waonyeshe mshikamano wao kwa kutompa kura Wambura katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, Dar es Salaam.
“Ile kamati ya Rufani, wajumbe watatu waliompigia kura za ndiyo Wambura ni Yanga wanaofahamika vizuri, Mwenyekiti Lugaziya, Juma Abeid Khamis na Rashid Dilunga, wawili waliomkataa ndiyo Simba , Mwita Waisaka na Masoud Isangu, sasa hii ni picha ambayo iko wazi kabisa kwamba huyu mtu si Simba mwenzetu, bali ni mpinzani wetu wa jadi, Yanga damu,”amesema Bedui.
Jana Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitangaza rasmi kumrejesha Wambura kugombea Urais wa Simba.
Hiyo ilifuatia Wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti Wakili Julius Lugaziya kupiga kura baada ya kushindwa kukubaliana juu ya uamuzi wa kuchukua..
Hata hivyo Wambura anatarajiwa kujadiliwa tena kesho Ijumaa katika Kamati ya Maadili kutokana na mwanachama wa Simba, Jackson Sagonge 'Chacha' kuwasilisha malalamiko yake katika kamati hiyo tangu wiki iliyopita.
Akitangaza maamuzi ya rufaa hiyo iliyojadiliwa kwa muda wa siku mbili Wakili Lugaziya, alisema kuwa baada ya kupitia hoja 14 na mapingamizi ya awali yaliyowasilishwa na mrufani (Wambura) na maelezo kutoka kwa wanachama watano waliomuwekea pingamizi wakiongozwa na Said Rubeya, waliamua kupiga kura.
"Uamuzi wa Kamati ya Rufaa ulizingatia wingi wa kura, kwa sababu wajumbe hawakukubaliana kwa kauli moja kupata muafaka wa rufaa hii," alisema Lugaziya kabla ya kueleza hoja ambazo kamati yake ilizijadili na kuamua kumrejesha Wambura kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa klabu hiyo.
Lugaziya alisema kuwa kamati yake imeamua kubatilisha uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba kwa sababu kuu nne ikiwano Wambura kuendelea kushiriki kulipa ada ya uanachama na mchango wa mawazo isipokuwa uchaguzi uliopita.
Alisema pia mrufani huyo alikuwa akishiriki mikutano mikuu ya klabu na ya dharura iliyoitishwa huku kikatiba mwanachama anayeruhusiwa kushiriki ni hai.
Aliongeza kwamba Wambura amerejeshwa kutokana na kuteuliwa kwenye Kamati ya kuandaa Mpango Mkakati wa wa klabu hiyo na mapema mwaka huu aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji inayomaliza muda wake.
"Kimatendo hakuna mahali panapoonyesha Wambura alisimamishwa, na kama yeye alikuwa si mwanachama halali basi vikao vyote alivyoshiriki ikiwamo cha marekebisho ya katiba na kuteua Kamati ya Uchaguzi navyo ni batili," Lugaziya aliongeza.
Alieleza pia suala na kusimamishwa uanachama halikuwahi kuhojiwa na mgombea huyo au mwanachama mwingine katika mkutano mkuu uliofuata na tangu alipoandikiwa barua ya kusimamishwa Mei 5 mwaka 2010 wakati tayari imefanyika mikutano minne na vikao vya kamati ya utendaji vilivyoanishwa katiba katiba 20.
Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kwamba uamuzi wa kamati yake hauwafungi wadau kwenda mahakamani kudai haki ila unaelenga kukumbusha klabu na wanachama wengine wa TFF kuzingatia taratibu walizojiwekea kwa weledi badala ya kutumia taratibu hizo kwa manufaa hasi katika mchezo wa soka hapa nchini.
Klabu ya Simba inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Juni 29 mwaka huu na viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa muda wa miaka minne na mgombea Urais anayeungwa mkono na wengi hadi sasa Evans Elieza Aveva.

![]() |
Mamluki? Wanachama wa Simba SC wanadai Michael Wambura anapandikizwa na wapinzani wao, Yanga SC |

0 comments:
Post a Comment