PAMOJA na kupelekwa kambini Chuo Kikuu cha Barry mini Miami, Marekani kwa maandalizi ya mwisho ya Kombe la Dunia, haikuwazuia wachezaji wa England kutoka kwenda madukani kufanya matanuzi.
Nahodha wa Three Lions, Steven Gerrard aliwaontoza wachezaki wenzake wakiwemo Glen Johnson, Phil Jagielka, Leighton Baines na Rickie Lambert kwenda maduka ya Bal Harbour kufanya manunuzi.
England itakuwa na mechi mbili za mwisho za kujipima kabla ya Kombe la Dunia nchini Brazil, ya kwanza wakicheza na Ecuador kesho na nyingine Jumamosi na Honduras.
Mabishoo mitaani: Nahodha Steven Gerrard akiwaongoza wachezaji wenzake wa England, Glen Johnson, Phil Jagielka, Leighton Baines na Rickie Lambert katika maduka ya Bal Harbour mjini Miami



.png)
0 comments:
Post a Comment