ITALIA imetangaza kikosi chake cha mwisho kwa ajili ya Kombe la Dunia, huku mshambuliaji Mario Balotelli akifanikiwa kubaki katika wachezaji 23.
Lakini mijadala inaendelea juu ya uteuzi wa kocha wa Azzurri, Cesare Prandelli haswa baada ya kumuacha mshambuliaji Giuseppe Rossi.
Babu yake Rossi, Bruno Petrocelli amekasirishwa na kitendo cha mjukuu wake, ambaye alipona majeruhi na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland iliyoisha kwa sare 0-0 Jumamosi kutemwa na kumuita kocha Prandelli msaliti.
Akihojiwa na kituo cha redio Italia, babu huyo alisema; “Siku mbili zilizopita Prandelli alisema maneno mengi mazuri, kisha saa 48 baadaye anabadilisha mawazo yake,”.
“Prandelli amefanya kosa kubwa sana, amemsaliti Rossi na hawezi kumuacha mtu kama mjukuu wangu ambaye ni mzima kabisa. Sitaishangilia Italia, kwa kuwa kuna wasaliti wa taifa. Nitashangilia Marekani,”.
“Huyu (Prandelli) si mzuri kiasi cha kutosha kumuhukumu mjukuu wangu na sina zaidi cha kusema. Nafahamu kwamba mjukuu wangu yuko fiti na ana vyeti vya vipimo vinavyothibitisha hilo,”alisema babu huyo.
Kikosi cha Italia kimepiga picha wachezaji wakiwa wamevalia suti nadhifu kama wapinzani wao kwenye kundi lao, England wakiwa kwenye kambi yao ya mazoezi, Florence.
Kikosi kamili cha Italia Kombe la Dunia ni makipa; Buffon (Juventus), Perin (Genoa) na Sirigu (Paris St. Germain), mabeki; Abate (Milan), Barzagli (Juventus), Bonucci (Juventus), Chiellini (Juventus), Darmian (Torino), De Sciglio (Milan) na Paletta (Parma).
Viungo ni; Aquilani (Fiorentina), Candreva (Lazio), De Rossi (Roma), Marchisio (Juventus), Thiago Motta (Paris St. Germain), Parolo (Parma), Pirlo (Juventus) na Verratti (Paris St. Germain) wakati washambuliaji ni Balotelli (Milan), Cassano (Parma), Cerci (Torino), Immobile (Torino) na Insigne (Napoli).

![]() |
| Balotelli katika suti ya Azzuri |
![]() |
| Wachezaji wa Italia katika suti nadhifu tayari kwa Kombe la Dunia |

.png)
0 comments:
Post a Comment