MABINGWA wa dunia, Hispania wameondoka jana kwenda Marekani wakiwa njiani kuelekea Brazil kutetea mwali wao.
Kikosi cha wachezaji 23 wa Vicente Del Bosque kimekwea ndege ya Iberia, ambayo ina jina la Mfalme Juan Carlos wa kwanza ikiwa imeandikwa: "Tumebeba matumaini ya taifa."
Kocha huyo mkongwe amesema morali ya timu ipo juu na ana matumaini makubwa ya kuwapa raha mashabiki wa Hispania kwa kurejea na Kombe.
Hispania amnbayo imeshinda mataji mataji mawili yaliyopita ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, inatarajiwa kuweka kambi ya muds ya mazoezi Washington, ambako watamenyana na El Salvador Jumamosi ya Juni 7.
Ndege iliyobeba wachezaji wa Hispania iki3a imepambwa kwa picha za mashabiki
Siku inayofuata, Hispania itasafiri kwenda kwenye kambi yao ya Kombe la Dunia, viwanja vya mazoezi vya Caju mjini Curitiba, ambako kwa kawaida hutumiwa na klabu ya Atletico Paranaense ya Brazil.
Watatembelewa na Rais wa Brazil, Dilma Rousseff, kabla ya mchezo wao wa ufunguzi kutetea Kombe la Dunia dhidi ya Uholanzi Juni 13.



.png)
0 comments:
Post a Comment