Na Mwandishi Wetu, YOUNDE
WACHEZAJI wawili wa Coton Sport, kipa Loic Fedjou na beki Cedric Djeugoue ndiyo pekee kati ya wachezaji wanaocheza nyumbani waliteuliwa katika kikosi cha mwisho cha Cameroon cha wachezaji 23 kitakachokwenda kwenye Fainali za Kombe kla Dunia Brazil.
Kocha Volker Finke baada ya mechi za kirafiki dhidi ya Macedonia, Paraguay na Ujerumani, amekata wachezaji watano ambao ni kipa Guy N’dy Assembe, mabeki Jean Armel Kana Biyik, Gaetan Bong, kiungo Raoul Loe na mshambuliaji mkongwe Mohammadou Iddrisou. Simba Wasiofungika wapo Kundi A pamoja na wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.
Mabingwa hao mara nne Afrika wataanza kampeni yao Juni 14 kwa kumenyana na Mexico mjini Natal, kabla ya kucheza na Croatia siku nne baadaye mjini Manaus kisha kumaliza na Brazil Juni 23 mjini Brasilia.
Kikosi kamili ni, makipa; Charles Itandje (Konyaspor/Uturuki), Sammy Ndjock ( Fethiyespor/ Uturuki), Loic Feudjou (Coton Sport/Cameroon), mabeki; Allan Nyom (Granada/Hispania), Dany Nounkeu (Besiktas/Uturuki), Cedric Djeugoue (Coton Sport/Cameroon), Aurelien Chedjou (Galatasaray/Uturuki), Nicolas Nkoulou (Marseille/ Ufaransa), Henri Bedimo (Lyon/Ufaransa), Benoit Assou- Ekotto (Queens Park Rangers /England).
Viungo ni; Eyong Enoh (Antalyaspor /Ururuki), Jean II Makoun (Rennes/Ufaransa), Joel Matip (Schalke/ Ujerumani), Stephane Mbia (Sevilla/Hispania), Landry Nguemo (Bordeaux/Ufaransa), Alexandre Song (Barcelona/Hispania), Edgar Sally (Lens/Ufaransa).
Washambuliaji ni; Samuel Eto'o (Chelsea/England), Eric Choupo -Moting (Mainz/Ujerumani), Benjamin Moukandjo (Nancy/Ufaransa), Vincent Abubakar (Lorient/Ufaransa), Achille Webo (Fenerbahce/Uturuki), Fabrice Olinga (SV Zulte/Ubelgiji).

.png)
0 comments:
Post a Comment