MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid wamefichua jezi mpya za msimu ujao na katika kuashiria hawatamuachia Karim Benzema anayetakiwa na Arsenal, naye ametumia katika matangazo ya jezi hizo.
Arsene Wenger amekuwa akimtaka kwa muda mrefu Mfaransa mwenzake huyo bila mafanikio na kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji walio katika mipango yake baada ya kusaini Mkataba mpya wa miaka mitatu.
Lakini katika tangazo la jezi mpya za vigogo hao wa Hispania, Gareth Bale na Karim Benzema wote wametumika.
Msimu ujao wa 2014-2015, Cristiano Ronaldo na wenzake wataendelea kuvaa jezi zao za asili, nyeupe kwa mechi za nyumbani, ugenini watakuwa wanavaa pinki. Rangi ya tatu ni bluu.



.png)
0 comments:
Post a Comment