• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 22, 2014

  YAYA TOURE APIGA HAT TRICK MAN CITY IKIUA 5-0 ENGLAND

  MANCHESTER City imerudi kwa hasira katika Ligi Kuu ya England ikitoka kutolewa Ligi ya Mabingwa Ulaya- baada ya jioni hii kuifumua mabao 5-0 Fulham katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester.
  Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure leo amepiga hat trick yake ya kwanza, mabao mawili akifunga kwa penalti dakika ya 26 na 54 na linguine dakika ya 65 akimalizia pasi ya Samir Nasri.
  Mabao mengine ya Man City yamefungwa na Fernandinho dakika ya 84, akimalizia pasi ya Milner na Demichelis dakika ya 88. Ushindi huo, unaifanya City ifikishe pointi 63 baada ya kucheza mechi 28 na kupanda nafasi ya tatu mbele ya Arsenal yenye pointi 62 za mechi 30. 
  Chelsea inaongoza Ligi Kuu England kwa pointi zake 69 za mechi 31, ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 65 baada ya mechi 30, wakati Arsenal yenye pointi 62 ni ya nne.
  Mtu wa furaha: Yaya Toure amefunga hat-trick leo Manchester City ikiilaza Fulham mabao 5-0
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YAYA TOURE APIGA HAT TRICK MAN CITY IKIUA 5-0 ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top