• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 21, 2014

  BONGE LA PIGO MAN UNITED, VAN PERSIE AUMIA GOTI NA ATAKUWA NJE WIKI SITA, ATAKOSA MECHI ZOTE NA BAYERN MUNICH

  MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Robin van Persie atakuwa nje kwa wiki sita baada ya kubainika maumivu aliyoyapata katika mechi na Olympiacos na makubwa kuliko ilivyofikiriwa.
  Van Persie alitolewa nje usiku wa Jumatano kwa machela Uwanja wa Old Trafford baada ya kupiga hat-trick siku ambayo United iliichapa Olympiacos 3-0 na kutinga Robo Fainali ya Mabingwa Ulaya.
  Pigo: Robin van Persie akitolewa nje kwa machela JUmatano usiku alipoifungia mabao yote matatu Man United dhidi ya Olympiacos

  MECHI ATAKAZOKOSA RVP

  Machi 23: West Ham (A)
  Machi 25: Man City (H)
  Machi 29: Aston Villa (H)
  Aprili 1: Bayern Munich (H)
  Aprili 5: Newcastle (A)
  Aprili 9: Bayern Munich (A)
  Aprili 20: Everton (A)
  Aprili 26: Norwich (H)
  (H ni mechi za nyumbani na A ni mechi za ugenini)
  Kocha wa United, David Moyes aliyachukulia poa maumivu hayo baada ya mechi na ilifikiriwa Van Persie atakosa mchezo mmoja tu wa Jumamosi dhidi ya West Ham - kabla ya kurejea katika pambano la mahasimu wa Jiji la Manchester usiku wa Jumanne.
  Lakini klabu hiyo imetweet: "Kufuatia uchunguzi wa kina, Robin van Persie ameumia goti, ambalo litamuweka nje kwa kiasi cha wiki nne hadi sita,".
  Pamoja na kukosa mechi dhidi ya West Ham na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Van Persie, ambaye amefunga mabao 17 msimu huu, atakosa pia mechi dhidi ya Manchester City Jumanne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BONGE LA PIGO MAN UNITED, VAN PERSIE AUMIA GOTI NA ATAKUWA NJE WIKI SITA, ATAKOSA MECHI ZOTE NA BAYERN MUNICH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top