• HABARI MPYA

    Thursday, March 20, 2014

    TFF YAOMBOLEZA KIFO CHA SHABIKI ALIYEKUFA YANGA NA AZAM TAIFA JANA

    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mshabiki Deodatus Mwakyangula kilichotokea jana (Machi 19 mwaka huu) wakati ya mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Msiba huo ni mkubwa kwa familia ya Mwakyangula na kwetu, kwani umetokea wakati akiwa uwanjani kushuhudia mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.

    TFF imetoa pole kwa familia ya marehemu Mwakyangula, na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
    Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAOMBOLEZA KIFO CHA SHABIKI ALIYEKUFA YANGA NA AZAM TAIFA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top