• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 29, 2014

  SAMATTA…SAMATTA..SAMATTAA, KILA KONA KONGO NZIMA NI SAMATTA TUUU…AIRUDISHA MAZEMBE NANE BORA LIGI YA MABINGWA

  Na Princess Asia, Lubumbashi
  KLABU ya TP Mazembe imefuzu kutinga Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sewe Sport ya Ivory Coast 1-0 jioni hii Uwanja wa Kamalondo mjini Lubumbashi.
  Mazembe imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia awali kufungwa 2-1 mjini Abidjan Jumapili iliyopita.
  Kifaa adimu; Mbwana Samatta ameirudisha Mazembe Nane Bora Ligi ya Mabingwa Afrika

  Alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta aliyefunga bao hilo pekee dakika za mwishoni kipindi cha pili na kuirudisha timu hiyo ya DRC kwenye hatua ya makundi tangu mwaka 2012 waliposhiriki mara ya mwisho.
  Samatta pia ndiye aliyefunga bao la Mazembe Abidjan ikifungwa 2-1 na maana yake yeye ndiye ameibeba kwa mabega yake timu hiyo hadi Nane Bora na sasa itasubiri kujua wapinzani wake watatu katika droo itakayopangwa Aprili 29 mjini Cairo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA…SAMATTA..SAMATTAA, KILA KONA KONGO NZIMA NI SAMATTA TUUU…AIRUDISHA MAZEMBE NANE BORA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top