• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 25, 2014

  DIAMOND AENDELEA KUPETA TUZO ZA KILI, ATENGEWA TUZO SITA 2014

  Na Saidy Mdoe, Dar es Salaam
  MWANAMUZIKI nyota nchini, Nassib Abdul 'Diamond Platinum' ameingia katika vipengele sita vya kinyan’ganyiro cha tuzo za muziki nchini, maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014.
  Kwenye muziki mama (dansi na taarab) kuna mchuano mkali katika vipengele vya mwimbaji bora, mtunzi bora, mwimbaji bora wa kiume, mwimbaji bora wa kike, kundi bora na bendi bora.
  Katika wimbo bora wa bendi Ushamba Mzigo (Mashujaaa Band), Shamba la Bibi (Victoria Sound), Chuki ya Nini (FM Academia), Yarabi Nafsi (Mapacha Watatu) na Kiapo Mara Tatu (Talent Band) zitachuana vikali huku kwenye wimbo bora wa taarab kutakuwa na Wasi wasi wako – Mzee Yussuf,  Nipe Stara – Rahma Machupa, Sitaki Shari – Leyla Ramadhan, Mambo Bado – Hadija Yussuf  (wote Jahazi Jahazi), Asiyekujua Hakuthamini – Isha Ramadhan na Saida Ramadhan (Mashauzi Classic), Fahari ya Mwanamke – Hadija Kopa (G5 Modern Taarab), Kila Muomba Mungu – Mwanahawa Ali (Five Stars Modern Taraab).
  Katika bendi bora za dansi ni Bendi ya mwaka , FM Academia, Mapacha Watatu, African Stars(Twanga Pepeta), Akudo Impact, Malaika Band, Mashujaa Band wakati kundi bora la taarab ni mchuano kati ya Jahaz Modern Taarab Mashauzi Classic na Five Stars.
  Pata wasaa wa kujionea mwenyewe vipenge vyote. Vipengele vilivyozidi washiriki watano imetokea kwa sababu ya watu kufungana kura wakati zile zenye pungufu ya tano ni kwasababu ya uchache wa washiriki wanaokidhi vigezo vya mwaka husika. 
  Saluti5 imegundua kuwa yapo makosa ya kiaundishi kwenye baadhi ya majina ambapo utakutana na makosa kadhaa katika orodha hii iliyoandaliwa na waandaaji. Kwa mfano kwenye watunzi bora wa taarab utakutana na makosa kama vile Thabit Abdul kuandikwa Sadiki Abdul, Alhad Omar kuandikwa El Ahadi Omar.
  Maswahiba; Diamond akiwa na mchezaji wa Yanga SC,Mrisho Ngassa. Mwanamuziki huyo ameingia tena katika tuzo za Kili mwaka huu, huu ukiwa ni mwaka wa tatu mfululizo 

  Wimbo bora wa mwaka; 1 Number one-Diamond, 2 Joto hasira-Lady Jaydee Ft Prof Jay, 3 I love u-Cassim Mganga, 4 Yahaya-Lady JayDee, 5 Kidela -Abdu Kiba Feat Ali Kiba na 6 Muziki gani-Ney ft Diamond.
  Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya Kitanzania; 1 Kwejaga nyangisha-Batarokota, 2 Nalonji-Kumpeneka, 3 Bora Mchawi-Dar Bongo massive, 4 Tumbo lamsokota-Ashimba, 5 Aliponji –Wanakijiji na 6 Agwemwana-Cocodo African music band.
  Wimbo bora wa kiswahili –Bendi; 1 Ushamba mzigo-Mashujaa Band, 2 Shamba la Bibi -Victoria Sound, 3 Chuki ya nini -FM Academia, 4 Yarabi nafsi -Mapacha Watatu na 5 Kiapo mara 3 -Talent Band.
  Wimbo bora wa Reggae; 1 Niwe na wewe-Dabo, 2 Hakuna Matata-Lonka, 3 Tell Me-Dj Aron ft Fidempha, 4 Bado nahitaji-Chikaka ft Bless p & Lazzy B na  5 Bongo Reggae-Warriors from the east.  
  Wimbo bora wa Afrika Mashashariki; 1 Tubonge-Jose Chamelleone, 2 Nakupenda Pia-Waire Ft Allain, 3 Badilisha-Jose Chamelleone, 4 Kipepeo-Jaguar na 5 Kiboko Changu-Aman FT Weizal and Radio.
  Wimbo bora wa Afro pop; 1 Number one-Diamond, 2 Joto hasira-Jay Dee, 3 Kidela-abdul kiba ft Ali Kiba, 4 I love you-Kassim, 5 Tupogo-Ommy Dimpoz Ft J Martins na 6 Roho yangu-Rich Mavoko.
  Wimbo bora wa Taarab; 1 Wasi wasi wako-Mzee Yusuf, 2  Asiyekujua Hakuthamini-Isha Ramadhani & Saida Ramadhani, 3 Nipe stara -Rahma Machupa, 4 Sitaki shari-Leyla Rashid, 5 Fahari ya Mwanamke-Khadija Kopa, 6 Mambo bado-Khadija Yusuf na 7 Kila muomba Mungu -Mwanahawa Ali.
  Wimbo bora wa Hip hop; 1 Bei ya mkaa-Weusi, 2 Nje ya box-Nick wa pili ft Joh Makini na Gnako, 3 Siri ya mchezo-Fid q ft Nature, 4 2030-Roma na 5 Pesa-Mr Blue Ft Becka Title.
  Wimbo bora wa R&B; 1 Listen-Belle 9, 2 Closer -Vanessa Mdee, 3 So crazy-Maua ft Fa, 4 kama huwezi-rama dee ft jay dee na 5 Wa ubani-Ben Pol ft. Alice
  Wimbo bora wa kushirikisha/kushirikiana; 1 Music Gani-Ney Mitego ft Diamond, 2 Joto Hasira-Lady JayDee ft. Prof Jay, 3 Kidela -Abdul Kiba ft. Ali Kiba, 4 Bila Kukunja Goti-Mwana FA na AY ft. Jay Martins na 5 Tupogo-Ommy Dimpoz ft. Jay Martins.
  Wimbo bora wa Ragga/Dancehall; 1 Nishai-Chibwa Ft Juru, 2 Sex girl-Dr Jahson, 3 My sweet-Jettyman Dizano, 4 Feel Alright-Lucky Stone, 5 Wine-Princess Delyla. 
  Wimbo bora wa Zouk /Rhumba; 1 Yahaya-Lady Jaydee, 2 Yamoto-Mkubwa na wanawe, 3 Msaliti-Christian Bella, 4 Nakuhitaji-Malaika Band na 5 Narudi kazini-Beka.
  Mwimbaji bora wa kike -kizazi kipya; 1 Vanessa Mdee, 2 Lady Jaydee, 3 Linah na 4 Maua, wakati Mwimbaji bora wa kiume -kizazi kipya 1 Ben Pol, 2 Rich Mavoko, 3 Diamond, 4 Ommy Dimpoz na 5 Cassim Mganga.
  Mwimbaji bora wa kike –Taarab; 1 Khadija Kopa, 2 Isha Ramadhani, 3 Khadija Yusuf, 4 Mwanahawa Ali na 5 Leyla Rashid, wakati Mwimbaji bora wa kiume –Taarab wanashindana 1 Mzee Yusuf, Hashimu Saidi na 3 Mohamedi Ali aka Mtoto Pori.
  Mwimbaji bora wa kiume –Bendi; 1 Jose Mara, 2 Kalala Junior, 3 Charz Baba, 4 Khalid Chokoraa na 5 Christian Bella, wakati Mwimbaji bora wa kike -Bendi wanashindana 1 Luiza Mbutu, 2 Catherine (Cindy) na 3 Ciana.
  Msanii bora wa -Hip hop; 1 FID Q, 2 Stamina, 3 Young killer (Msodoki), 4 Nick wa pili, 5 Gnako.
  Msanii bora chipukizi anayeibukia; 1 Young Killer(Msodoki), 2 Walter Chilambo,  3 Y Tony,  4 Snura na 5 Meninah, wakati Rapa bora wa mwaka –Bendi kuna 1 Kitokololo, 2 Chokoraa, 3 Furguson, 4 Canal Top na 5 Totoo ze Bingwa.
  Mtumbuizaji bora wa kike wa Muziki. 1 Khadija Kopa, 2 Vanessa Mdee, 3 Isha Ramadhani, 4 Luiza Mbutu na 5 Catherine (Cindy), wakati Mtumbuizaji bora wa kiume wa Muziki 1 Diamond, 2 Christian Bella, 3 Rich Mavoko, 4 Ommy Dimpoz na 5 Abdu Kiba.
  Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka –Taarab; 1 Enrico, 2 Ababuu Mwana ZNZ na 3 Bakunde, wakati 
  Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka -Kizazi kipya wanachuana 1 Marco chali-Mj Records, 2 Man Water-Combination Sound, Mazoo-Mazoo Records, 4 Sheddy Clever-Burnz Records na 5 Nahreel -Home Town Record.
  Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka –Bendi; 1 Allan Mapigo, 2 C9, 3 Enrico, 4 Amoroso na 5 Ababuu Mwana ZNZ, wakati Mtunzi bora wa mwaka –Taarabu, 1  Mzee Yusuf, El-Ahad Omary, 3 El-khatib Rajab, 4 Kapten Temba, 5 Sadiki Abdul
  6 Nassoro Seif, Mtunzi bora wa mwaka -kizazi kipya, 1 Belle 9, 2 Ben Pol, 3 Diamond, 4 Rama dee 5 Rich mavoko.
  Mtunzi bora wa mwaka –Bendi wanachuana, 1 Christia Bella, 2 Jose Mara, 3 Chaz Baba, 4 Nyoshi Saadat na 5 Kalala Junior, wakati Mtunzi bora wa mwaka -Hip hop, 1 Nikki wa Pili, 2 Young Killer(Msodoki), 3 Roma,  4 FID Q na 5 G- Nako.
  Video bora ya muziki ya mwaka; 1 Number One-Diamond, 2 Yahaya-lady Jaydee, 3 Joto hasira-Lady Jaydee Ft Prof Jay, 4 Uswazi takeaway-Chege Ft Malaika, 5 Mama Yeyo-Gnako Ft Ben Pol.
  Bendi bora ya mwaka; 1 FM Academia, 2 Mapacha Watatu, 3 African Stars ‘Twanga Pepeta’, 4 Akudo Impact, 5 Malaika Band, 6 Mashujaa Band, wakati Kikundi cha mwaka cha Taarab ni 1 Jahaz Modern Taarab, 2 Mashauzi Classic na 3 Five Stars na Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya; 1 Makomandoo 2 Navy kenzo, 3 Weusi4 Mkubwa na wanawe
  (CHANZO: www.saluti5.com).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DIAMOND AENDELEA KUPETA TUZO ZA KILI, ATENGEWA TUZO SITA 2014 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top