• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 24, 2014

  AZAM FC WAIFUATA JKT MGAMBO KWA NGUVU ZOTE KUBEBA POINTI ZA UBINGWA

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  AZAM FC inaondoka Dar es Salaam kesho asubuhi kwa basi lake kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mgambo JKT Jumatano Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.
  Kocha Joseph Marius Omog raia wa Cameroon leo amewapa wachezaji wake mapumziko baada ya mechi ngumu ya jana wakishinda 1-0 dhidi ya JKT Oljoro, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, lakini jioni watafanya mazoezi mepesi.

  Baada ya mazoezi hayo, wachezaji wa Azam watalala kambini katika hosteli zao za Azam Complex tayari kudamkia safari ya kesho mapema.
  Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba timu itaondoka mapema kesho ili iwahi kufika safari hiyo ya takrban saa nne barabarani, wachezaji wapumzike kabla ya kufanya mazoezi Uwanja wa Mkwakwani jioni. 
  Jemadari amesema kwamba wachezaji ambao hawatahusika katika safari hiyo ya kufuata pointi tatu muhimu kwenye mbio za ubingwa ni majeruhi, Samih Haji Nuhu, Joseph Lubasha Kimwaga, Ibrahim Mwaipopo, Farid Mussa na Ismail Gambo.
  Timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Bakhresa  jana ilipiga hatua kuikimbia Yanga SC katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya baada ya kuifunga JKT Oljoro bao 1-0 jioni hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Matokeo hayo yanaifanya Azam FC itimize pointi 47 baada ya kucheza mechi 21, ikiwazidi mabingwa watetezi, Yanga SC kwa pointi nne ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Shujaa wa Azam FC jana alikuwa ni John Bocco ‘Adebayor’ aliyefunga bao hilo peke dakika ya 71 kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya kinda Kevin Friday. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC WAIFUATA JKT MGAMBO KWA NGUVU ZOTE KUBEBA POINTI ZA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top