• HABARI MPYA

  Monday, March 31, 2014

  SIMBA NA AZAM YAINGIZA MILIONI 26

  Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
  MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Machi 30 mwaka huu) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza sh. 26,455,000.
  Watazamaji 4,741 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
  Kiungo wa Azam FC, Kipre Balou kulia akimtoka kiungo wa Simba SC, Henry Joseph jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Azam ilishinda 2-1.

  Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akimtoka beki wa Simba SC, Donald Mosoti 

  Mgawanyo kwa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,035,508.47, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,908,686 wakati kila klabu ilipata sh. 5,460,687.63.
  Uwanja sh. 2,776,620.83, gharama za mechi sh. 1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh. 1,665,972.50, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 832,986.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 647,878.19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA AZAM YAINGIZA MILIONI 26 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top