• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 23, 2014

  BAYERN MUNICH BADO MECHI MOJA TU KUTANGAZA UBINGWA BUNDESLIGA WAKATI LIGI BADO MBICHI

  MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich wameendeleza wimbi la ushindi katika Bundesliga baada ya ushindi wa mabao 2-0 jana dhidi ya Mainz na sasa inahitaji kushinda mechi moja zaidi ili kujihakikishia taji hilo la Ligi Kuu ya Ujerumani. 
  Bastian Schweinsteiger alifunga bao la kwanza dakika ya 82 kabla ya Mario Gotze aliyetokea benchi kufunga la pili dakika nne baadaye wakiiwezesha Bayern kuweka rekodi ya kushinda mechi 18 mfululizo na kutimiza mechi 51 za kucheza bila kupoteza. 
  Borussia Dortmund wanaoshika nafasi ya pili wameshinda mabao 3-0 jana dhidi ya Hannover, lakini wanaendelea kuzidiwa pointi 23 na Bayern zikiwa zimebaki mechi nane ligi kufikia tamati.

  Mchezo umeisha: Mario Gotze akishangilia baada ya kufunga bao la pili jana 
  Unbelievable: Bayern Munich players celebrate after the final whistle after making it 51 games unbeaten
  Ngumu kuamini: Wachezaji wa Bayern Munich wakisherehekea kucheza mechi ya 51 bila kupoteza jana

  Bayern inaweza kutwaa kuweka rekodi ya kutwaa taji mapema zaidi miaka 51 ya Bundesliga iwapo itashinda dhidi ya Hertha Berlin Jumanne, kutegemeana na matokeo ya Dortmund ambao jioni hiyo hiyo watacheza na Schalke.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BAYERN MUNICH BADO MECHI MOJA TU KUTANGAZA UBINGWA BUNDESLIGA WAKATI LIGI BADO MBICHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top