• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 31, 2014

  AY AKAMILISHA VIDEO YA ASANTE, IMEPAMBWA NA MODO WA KENYA

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam 
  AMBWENE Yesaya au AY amekamilisha video ya wimbo wake uitwao Asante na sasa utaanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya Redio na Televisheni nchini.
  AY ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, video hiyo imerekodiwa na Kevin Bosco Jr Productions ya Kenya nchini humo na zaidi ya yeye mwenyewe kuna binti mmoja tu mwanamitindo wa Kenya.
  AY amekamilisha video ya wimbo Asante

  “Ni video fulani yaani siwezi kuielezea, ni mtu uione mwenyewe, tamu sana”alisema AY katika hoteli ya Double Tree, Masaki, Dar es Salaam alikohudhuria semina ya wanamuziki walioingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Kili 2014.  
  Ikumbukwe wimbo huo uliorekodiwa studio za MJ Productions na Marco Chali Februari mwaka huu na umekuwa ukifanya vizuri kwenye stesheni mbalimbali za Redio Afrika Mashariki na Kati tangu wakati huo. 
  Katika wimbo huo, AY amemshirikisha binti aitwaye Dela, lakini pia amehusisha sauti za Diamond na Jade.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AY AKAMILISHA VIDEO YA ASANTE, IMEPAMBWA NA MODO WA KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top