• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 27, 2014

  FIFA KUWEKA NYASI BANDIA UWANJA WA KAITABA

  SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limekubali kuweka nyasi bandia katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, wamepokea taarifa ya FIFA ikisema imekubali ombi la kugharamia uwekaji nyasi bandia Uwanja wa Kaitaba.
  “TFF inalishukuru Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa kukubali kugharamia uwekaji nyasi za bandia kwenye Uwanja wa Kaitaba, na pia kusaidia uendelezaji wa uwanja wa TFF wa Tanga,”amesema.
  Rais wa FIFA, Sepp Blatter   

  Mbali na kuwa Rais wa TFF, Malinzi pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Bukoba (KRFA) na Uwanja wa Kaitaba kwa muda mrefu umekuwa katika hali ya mbaya, kiasi cha kulalamikiwa na timu zinazokwenda kucheza huko na imekuwa ngome kuu ya wenyeji katika Ligi Kuu, Kagera Sugar kuvunia pointi kutokana na kuuzoea Uwanja huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FIFA KUWEKA NYASI BANDIA UWANJA WA KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top