• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 21, 2014

  SAMATTA NA ULIMWENGU WATUA IVORY COAST TP MAZEMBE IKIWA KAZINI LIGI YA MABINGWA

  Na Prince Akbar, Dar es Salaam
  TOUT  Puisant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tayari wapo Abidjan, Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Sewe Sport jioni ya kesho.
  Timu hiyo yenye washambuliaji wawili wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu imekuwa na habati kuanzia ugenini hatua hiyo, kama itapata matokeo mazuri ya awali, itafurahia kucheza mechi ya marudiano mbele ya mashabiki wake wenye sapoti kubwa mjini Lubumbashi.
  Wawakilishi wa nchi Ligi ya Mabingwa; Mbwana  Samatta kulia na Thomas Ulimwengu kushoto wataendelea kulifanya jina Tanzania liendelee kutajwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa na jezi za TP Mazembe ya DRC

  Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri walioitoa Yanga SC kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya 1-1, wao pia wataanzia ugenini kesho dhidi ya Ahly Benghazi ya Libya.
  Horoya ya Guinea itaanzia nyumbani na CS Sfaxien ya Tunisia, sawa na ES Setif ya Algeria itakayoikaribisha Coton Sport ya Cameroon, AC Leopards ya Kongo itakayoikaribisha Al-Hilal ya Sudan na Nkana ya Zambia itakayoikaribisha Zamalek ya Misri.
  Timu nyingine ya DRC, AS Vita itaanzia nyumbani na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Uwanja wa Tata Raphael mjini Kinshasa, wakati mechi zote za marudiano zitachezwa Jumamosi ya Machi 29, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA NA ULIMWENGU WATUA IVORY COAST TP MAZEMBE IKIWA KAZINI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top