• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 30, 2014

  MOURINHO SASA AWAGEUKIA MADOGO WAOKOTA MIPIRA, ASEMA WANATUMIWA KUIKOSESHA CHELSEA UBINGWA

  KOCHA Jose Mourinho amewalalamikia waokota mipira wanatumiwa kukwamisha kampeni za Chelsea kutwaa ubingwa na kiasi fulani amekata tamaa za kutwaa taji la Ligi Kuu ya England licha ya kuwa kileleni.
  Hiyo inafuatia kipigo cha jana cha bao 1-0 kutoka kwa Crystal Palace Uwanja wa Selhurst— na akasema watu wanawafundisha watoto kuchelewesha kuwapa mipira ya kurusha wachezaji wa Chelsea akitolea mfano tukio la jana alilolazimika kuingilia.
  Zaidi ya hapo hakuwa na mengi ya kusema, sana kuwapongeza mabeki wake kama John Terry, aliyejifunga dakika ya 52 jana kuwapa ushindi Palace. 
  Lakini alipoulizwa ubora gani Chelsea inahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, Mourinho alichukua kipande cha karatasi na kuandika: 'mipira'.
  Kupagawa noma: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alimvaa muokota mipira wa Crystal Palace jana
  Calmed down: Mourinho was later pictured putting his arm around the Crystal Palace youngster
  Tulia kijana: Mourinho akimpa maneno kinda huyo wa Crystal Palace 

   Mourinho alimfuata muokota mipira wa Crystal ambaye alichelewesha kurudisha uwanjani mpira uliotoka mwishoni mwa mchezo na akasema alihofia isije kutokea kama ya Eden Hazard alipotolewa kwa kadi nyekundu kwa kumpiga muokota mipira wa Swansea msimu uliopita. 
  "Nilifikiri Cesar Azpilicueta alikuwa amepandwa na jazba na angeshindwa kujizuia (kwa muokota mipira) na yule mtoto amefundishwa kufanya hivyo, ikiwa mchezaji atampiga muokota mpira, wakati huo mtu yule mtu aliyemfundisha huyo mtoto hayu mtoto na mchezaji anapata matatizo kwa kumsukuma au kumpiga kijana. 
  "Nilikuwa nipo katika nafasi ya kumfikia yule mtoto na yule mtoto alikuwa mzuri na nilimuambia; “wewe fanya hivi, siku moja mtu mwingine atakupiga”. Tuliona kilichotokea kwa Eden,"alisema Mourinho.Honest: Jose Mourinho wrote down 'balls' when asked what quality his Chelsea side needed
  Ukweli: Jose Mourinho aliandika 'mipira' alipoulizwa ubora gani Chelsea inahitaji kutwaa ubingwa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOURINHO SASA AWAGEUKIA MADOGO WAOKOTA MIPIRA, ASEMA WANATUMIWA KUIKOSESHA CHELSEA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top