• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 26, 2014

  AZAM FC WAENDELEA KULA BATA KILELENI LIGI KUU, WAITANDIKA MGAMBO ISIYOFUNGIKA MKWAKWANI 2-0

  Na Saada Akida, Tanga
  AZAM FC  inaendelea kujinafasi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-0 jioni hii dhidi ya Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  Ushindi huo, unaifanya Azam ifikishe pointi 50 baada ya kucheza mechi 22 na kubaki kileleni mwa Ligi Kuu, mbele ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21. 
  Mabao ya Azam FC hii leo yamefungwa na washambuliaji wake, John Bocco dakika ya 63 kwa shuti kali akimalizia pasi ya Mganda, Brian Umony  aliyeingia dakika ya 53 kuchukua nafasi ya Gaudence Mwaikimba. 

  Bao la pili lilifungwa na Umony dakika ya 82 kwa shuti kali ambalo lilimbabatiza kipa Salehe Tendega na kuingia nyavuni.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Gaudence Mwaikimba/Brian Umony dk53 , John Bocco ‘Adebayor’ na Kipre Tchetche/Waziri Salum dk81.
  Mgambo JKT; Salehe Tendega, Bashiru Chanache, Salim Gilla, Salum Kipanga/Salum Malima dk28, Bakari Mtama, Novart Lulunga, Mohamed Samatta/Nassor Gumbo dk78, Peter Mwalyanzi, Fully Maganga, Bolly Shaibu/Mohammed Neto dk35 na Malimi Busungu.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC WAENDELEA KULA BATA KILELENI LIGI KUU, WAITANDIKA MGAMBO ISIYOFUNGIKA MKWAKWANI 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top