• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 27, 2014

  KONDA AITEKETEZA REAL MADRID LA LIGA NA KUIPOROMOSHA HADI NAFASI YA TATU, ATLETICO NA BARCA ZAUA NA KUPAA JUU

  MWANASOKA bora wa dunia, Christiano Ronaldo alimkasirikia Gareth Bale jana wakati Real Madrid ikifungwa kwa mara ya pili ndani ya siku nne katika La Liga na kupigwa kumbo na Barcelona na Atletico Madrid katika mbio za ubingwa.
  Huku Real ikichapwa mabao 2-1 na Sevilla, Ronaldo alishindwa kuficha hasira zake baada ya mwanasoka ghali duniani, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86, Bale alipoamua kupiga mpira wa adhabu, badala ya kumuachia mshambuliaji huyo Mreno, na akaenda kupiga juu ya lango.
  Ronaldo lionyeshwa na kamera za TV akimuwakia Bale baada ya kupiga ovyo faulo hiyo.
  Unatuzingua mwana: Cristiano Ronaldo akimuwakia Gareth Bale baada ya nyota huyo wa Wales kupiga ovyo faulo
  Real Madrid's Welsh forward Gareth Bale
  Real Madrid's Gareth Bale from Wales reacts during their La Liga match against Sevilla
  Nani, mimi? Bale aliwakiwa na Ronaldo aliyepagawa na kipigo cha pili Real Madrid 

  La Liga table
  Ilikuwa ni siku mbaya kwa mwanasoka huyo wa Wales, ambaye alitoka uwanjani mara moja kwenda kubadilisha viatu na kuiacha Real ikiwa pungufu na wachezaji 10. Wakati anabadilisha viatu, Carlos Bacca ndipo alipoifungia bao la ushindi Sevilla dakika ya 73.
  Kipigo cha Madrid Uwanja wa Sanchez Pizjuan jana, kinakuja siku nne baada ya kufungwa na Barcelona, Lionel Messi akimfunika Ronaldo kwa kufunga hat trick katika ushindi wa 4-3 mjini Madrid. 
  Vipigo hivyo mfululizo,vinakuja baada ya timu ya Carlo Ancelotti kucheza mechi 31 mfululizo bila kupoteza hata moja. 
  "Tunatakiwa kuendelea kufanya kazi, kupambana na kuwaomba msamaha mashabiki wetu,"alisema beki wa pembeni wa Madrid, Marcelo. 
  Unhappy: Ronaldo can't hide his frustration as Real Madrid slip to defeat at Sevilla
  Hana furaha: Ronaldo alishindwa kuficha hisia zake wakati Real Madrid ikifungwa na Sevilla
  Angry: Cristiano Ronaldo
  Bacca alikuwa kondakta wa basi za nchini mwao mwanzoni mwa umri wake wa miaka ya 20,kabla ya mambo kumnyookea kwenye soka.
  Mshambuliaji huyo wa Columbia alitua Sevilla kwa Pauni Milioni 6 msimu huu na sasa amekwishafunga mabao 18 kwenye mashindano yote msimu huu. 
  Alikuwa shujaa wa mchezo baada ya kipindi cha kwanza pia kufunga bao la kwanza dakika ya 19 kwa pasi ya Jose Antonio Reyes na kipindi cha pili alifunga kwa pasi ya Ivan Rakitich, kiungo wa Croatia aliyemtoka vizuri Pepe na kumpasia Bacca aliyemtungua kipa Diego Lopez kukamilisha ushindi wa 2-1. Ronaldo alifunga bao la Real dakika ya 14.
  Huku Atletico Madrid ikiifunga Granada 1-0, bao pekee la Diego Costa dakika ya 63, nayo Barcelona iliitandika 3-0 Celta mabao ya Neymar dakika ya sita na 67 na Messi dakika 30.
  Matokeo hayo, yanaifanya Atletico inayofundishwa na kocha Diego Simeone ipae kileleni mwa Liga kwa kufikisha pointi 73, Barcelona iliyofikisha pointi 72 sasa ya pili na Real inayobaki na pointi zake 70 inakuwa ya tatu. 
  Head over heels: Ronaldo takes a tumble under challenge from Sevilla's Stephane M'Bia
  Soka, au mapigano; Ronaldo akipambana na mchezaji wa Sevilla, Stephane M'Bia
  The winner: Bacca slots the ball underneath Real Madrid keeper Diego Lopez
  La ushindi: Bacca akimtungua kipawa Real Diego Lopez, kuifungia bao la ushindi timu yake
  Off course: Former bus conductor inflicted Real's second defeat in four days
  Ndiyo maana yake: Kondakta wa basi wa zamani akishangilia baada ya kuiua Real jana
  Goals: Two goals from Neymar and one from Lionel Messi did the damage for Barcelona against Celta Vigo
  Mabao: Mabao mawili ya Neymar na moja la Lionel Messi yameirejesha rasmi Barcelona kwenye mbio za ubingwa
  Deadly: Diego Costa scored the winner for Atletico Madrid against Granada
  Mkali hatari: Diego Costa ameifungia bao la ushindi Atletico Madrid dhidi ya Granada
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KONDA AITEKETEZA REAL MADRID LA LIGA NA KUIPOROMOSHA HADI NAFASI YA TATU, ATLETICO NA BARCA ZAUA NA KUPAA JUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top