• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 22, 2014

  CHELSEA YAIFANYA KITU MBAYA ARSENAL KATIKA MECHI YA 1,000 YA WENGER

  GHARIKA. Jose Mourinho amempa mechi ya 1,000 chungu Arsene Wenger baada ya Chelsea kuigaragaza Arsenal mabao 6-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni hii Uwanja wa Stamford Bridge, London.
  Siku moja baada ya Wenger kukabidhiwa tuzo ya dhahabu kwa kuiongoza Arsenal katika mechi 1,000 tangu aanze kazi, leo alitoka Uwanja wa Stamford Bridge akiwa kichwa chini na asiye na hamu kwa kipigo kikali kutoka kwa wapinzani wao hao kwenye mbio za ubingwa.
  La kwanza mapema: Samuel Eto'o akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza Stamford Bridge

  Mcameroon Samuel Eto’o alitangulia kuifungia The Blues dakika ya tano kwa pasi ya Andre Schurrle, ambaye yeye mwenyewe akafunga la pili dakika ya saba kwa pasi ya Nemanja Matic kabla ya Edin Hazard kufunga kwa penalti dakika ya 17.
  Penalti hiyo ilifuatia Alex Oxlade-Chamberlain kuushika mpira kwa makusudi akiokoa shuti la Edin Hazard, lakini ajabu refa akampa kadi nyekundu Kieran Gibbs.
  Zikiwa zimesalia dakika tatu kabla ya mapumziko, Oscar aliifungia Chelsea bao la tatu kwa pasi ya Fernando Torres, ambaye naye alipokea krosi ya Andre Schurrle.
  Kipindi cha pili, Chelsea walirudi na moto ule ule na dakika ya 66 Oscar aliifungia The Blues bao la tano kwa shuti la kawaida akiwa ndani ya eneo la hatari, ambalo lilionekana kama kipa Szczesny angeweza kuokoa, lakini akatunguliwa, kabla ya Mohamed Salah kufunga la sita dakika ya 71.
  Kwa matokeo hayo, Chelsea inazidi kujiwekea zege kileleni kwa kutimiza pointi 69 baada ya mechi 31 na Arsenal inabaki na pointi zake 62 baada ya mechi 30. 
  Running on: Schurrle stretches for the ball as Sagna looks on at Stamford Bridge
  Running on: Schurrle stretches for the ball as Sagna looks on at Stamford Bridge
  Captured: Szczesny dives at the feet of Fernando Torres as the strike slipped through
  Captured: Szczesny dives at the feet of Fernando Torres as the strike slipped through
  The boss: Arsenal fans hold up a sign to mark Arsene Wenger manager of his 1000th game at the club
  The boss: Arsenal fans hold up a sign to mark Arsene Wenger manager of his 1000th game at the club
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAIFANYA KITU MBAYA ARSENAL KATIKA MECHI YA 1,000 YA WENGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top