• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 22, 2014

  SUAREZ APIGA TATU PEKE YAKE LIVERPOOL IKITANDIKA MTU SITA

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez amepiga hat trick timu yake, Liverpool ikiifunga mabao 6-3 Cardiff City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni Uwanja wa Cardiff.
  Cardiff walitangulia kupata bao dakika ya tisa mfungaji Mutch kwa pasi ya Campbell, lakini Luis Suarez akaisawazishia Liverpool dakika ya 16 kwa pasi ya Johnson.
  Campbell aliifungia bao la pili Cardiff dakika ya 25 pasi ya Mutch na Martin Skrtel akaifungia Liverpool mara mbili mfululizo dakika ya 41 na 54, mabao yote pasi za Philippe Coutinho kabla ya Suarez kufunga la nne dakika ya 60 akimalizia pasi ya Daniel Sturridge.
  Sturridge alifunga bao la tano dakika ya 75 kwa pasi ya Suarez kabla ya  Mutch kuifungia Cardiff la tatu dakika ya 88, pasi ya Jones. Suarez alikamilisha hat trick yake dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida kwa bao la sita akimalizaia pasi ya Skrtel.
  Liverpool sasa inatimiza pointi 65 baada ya mechi 30 na kupanda hadi nafasi ya pili, ikiishusha Arsenal yenye pointi 62, huku Chelsea iking’ara kileleni kwa pointi zake 69 za mechi 31 na Manchester City ni ya tatu kwa pointi zake 63 za mechi 28.
  Furaha tupu: Luis Suarez kushoto akishangilia na Daniel Sturridge kulia
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUAREZ APIGA TATU PEKE YAKE LIVERPOOL IKITANDIKA MTU SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top