• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 21, 2014

  SPURS NJE ULAYA, ENGLAND HASARA TUPU MWAKA HUU

  ENGLAND haitakuwa na timu katika Robo Fainali ya Europa League kufuatia Tottenham Hotspur jana kutolewa na Benfica ya Ureno kwa jumla ya mabao 5-3, baada ya usiku wa jana kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Luz.
  Spurs ilifungwa 3-1 nyumbani katika mchezo wa kwanza na sasa inaungana na Swansea kuipa mkono wa kwaheri michuano hiyo.
  Katika mechi nyingine za Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, Valencia imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-0 dhidi ya Ludogorets baada ya jana kushinda 1-0 nyumbani, ikianza kushinda 3-0 ugenini, wakati Napoli imeaga kwa kipigo cha jumla cha 3-2 kufuatia jana kufungwa 1-0 na Porto ikitoka kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani katika mchezo wa kwanza.
  FC Basel imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Salzburg baada ya sare ya 0-0 jana nyumbani, ikitoka kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza ugenini, wakati Anzhi nayo imeaga kwa kipigo cha jumla cha 1-0 walichokipata katika mchezo wa kwanza ugenini na jana kutoa sare ya bila kufungana.
  Viktoria Plzen imeaga kwa jumla ya mabao 5-3 dhidi ya Olympique Lyon baada ya jana kushinda 2-1, wakati mchezo wa kwanza ilifungwa 4-1, Fiorentina imetolewa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya jana kufungwa 1-0 na Juventus nyumbani, ikitoka kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Sevilla imefuzu kwa penalti baada ya sare ya jumla ya 2-2 na Real Betis, kila timu ikishinda 2-0 nyumbani kwake.

  Nje: Wachezaji wa Spurs, Sandro (kushoto) na Christian Eriksen wakiwa wanyonge baada ya kutolewa katika Europa League jana na Benfica
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SPURS NJE ULAYA, ENGLAND HASARA TUPU MWAKA HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top