• HABARI MPYA

    Thursday, March 20, 2014

    MADADI MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI TFF

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam 
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemteua Salum Madadi kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Ufundi.
    Uteuzi huo umefanya na Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
    Kabla ya uteuzi, Madadi alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Januari mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Ufundi aliyekuwepo kumaliza mkataba wake Desemba 31 mwaka jana.
    Anaingia ofisini; Salum Madadi Mkurugenzi mpya wa Ufundi wa TFF


    Anaachia ofisi; Sunday kushoto Kayuni alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF kabla ya Madadi
    Madadi mwenye leseni A ya ukocha ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ni kocha mwenye uzoezi wa zaidi ya miaka 30 ambapo alianza kufundisha mpira wa miguu mwaka 1980 katika klabu ya Maji SC ya Lindi.
    Ana elimu ya sekondari aliyoipata katika shule ya Chidya na diploma ya ukocha wa mpira wa miguu aliyoipata nchini Ujerumani. Pia ni Mkufunzi wa makocha wa CAF, na alijiunga na TFF mwaka 2006 akiwa Ofisa Maendeleo.
    Alikuwa Kocha wa Taifa Stars mwaka 2000. Mbali ya Maji SC, amewahi kufundisha timu za Nyota Nyekundu, Ushirika ya Moshi, Simba, Shangani ya Zanzibar, Malindi ya Zanzibar, Cardif ya Mtwara na Kariakoo ya Lindi.
    Pia amewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
    Wakati huo huo: CAF imewateua Watanzania Alfred Rwiza na Leslie Liunda kusimamia mechi zake za wikiendi hii na mwezi ujao.
    Liunda ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) kati ya How Mine ya Zimbabwe na Bayelsa United ya Nigeria itakayochezwa Jumamosi (Machi 22 mwaka huu) jijini Bulawayo.
    Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Eritrea, na wanaongozwa na Maeruf Kherseed. Wasaidizi wake ni Angeson Ogbamariam, Berhe O’Michael na Luelseghed Ghebremichael.
    Naye Rwiza atasimamia mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Lesotho na Swaziland itakayochezwa kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Maseru.
    Mechi hiyo ya marudiano itachezwa na waamuzi Duncan Lengani, Innocent Kaundula, Hendrix Maseko na Jones Makhuwira, wote kutoka nchini Malawi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MADADI MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top