• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 30, 2014

  REAL YAUA 5-0 LA LIGA, LAKINI BADO YA TATU TU...BALE APIGA MBILI NA KURUDISHA USWAHIBA WAKE NA RONALDO

  NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale walirejesha urafiki wao tena wakati timu yao ikiifumua mabao 5-0 Rayo Vallecano usiku huu katika mchezo wa La Liga uliofanyika Uwanja wa Santiago Bernabeu.
  Bale alimsetia Ronaldo kuifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya 14, na akachangia bao la pili lililofungwa na Carvajal dakika ya 54, kabla ya kufunga la tatu dakika ya 67 na la nne dakika ya 70 wakati Morata alifunga la tano dakika ya 77. 
  Real sasa inatimiza pointi 73 baada ya mechi 31, lakini inaendelea kuketi nafasi ya tatu nyuma ya Barcelona yenye pointi 75 na Atletico Madrid pointi 76 kileleni, zote zikiwa zimecheza mechi 31 pia.
  Ronaldo alimkasirikia Bale baada ya kwenda kupiga mpira wa ovyo dakika za mwishoni Real ikilala 4-3 mbele ya Barcelona wiki iliyopita, lakini leo amemaliza hasira za mchezaji mwenzake huyo na kurudisha urafiki wao tena.
  Konde hilo: Gareth Bale akishangilia baada ya kuifungia Real katika ushindi wa 5-0Breakthrough: Cristiano Ronaldo celebrates after putting Real ahead on 14 minutes, his 28th La Liga goal of the season
  Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real bao lake la 28 katika msimu huu wa La Liga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL YAUA 5-0 LA LIGA, LAKINI BADO YA TATU TU...BALE APIGA MBILI NA KURUDISHA USWAHIBA WAKE NA RONALDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top