• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 30, 2014

  YA BABU WA YANGA YAMETIMIA, AL AHLY WATEMESHWA MZIGO, WAKUNGUTWA TATU NYUMBANI NA WALIBYA

  Na Salum Esry, Cairo
  UTABIRI wa kocha Mkuu wa Yanga SC, Hans van der Pluijm umetimia- baada ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri kutolewa Hatua ya 16 Bora kwa kipigo cha mabao 3-2 nyumbani jana na Al Ahly Benghazi ya Libya.
  Babu Mholanzi wa Yanga SC baada ya kutolewa na Al Ahly kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya 1-1 mapema mwezi huu, akasema hiyo siyo Al Ahly anayoijua, imeporomoka sana na kwa aina ya soka yake haitafika mbali.
  Wameaga; Al Ahly imevuliwa ubingwa wa Afrika baada ya jana kutolewa na Ahly Benghazi ya Libya 

  Kweli, Mashetani hao Wekundu wa Cairo wenye mataji nane ya Ligi ya Mabingwa wameaga kwa kipigo cha jumla ya mabao 4-2, baada ya awali pia kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza mjini Tunis.
  Mchezo wa kwanza ulifanyika Tunisia kwa sababu za kiusalama nchini Libya hivi sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YA BABU WA YANGA YAMETIMIA, AL AHLY WATEMESHWA MZIGO, WAKUNGUTWA TATU NYUMBANI NA WALIBYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top