• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 30, 2014

  MESSI AIPAISHA BARCA LA LIGA, REAL YAJIKONGOJA

  MSHAMBULIAJI Leo Messi amevunja mwiko wa kutowafunga Espanyol kwenye Uwanja wao wa Cornella El Prat baada ya usiku huu kuifungia bao pekee Barcelona dhidi ya wenyeji wao hao.
  Messi hakuwahi kufunga katika Uwanja huo katika misimu mitano, lakini leo hakufanya makosa alipokwenda kupiga penalti baada ya beki wa pembeni, Javi Lopez kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
  Barcelona sasa inafikisha pointi 75 baada ya mechi 31 na inaendelea kukaa nafasi ya pili nyuma ya Atletico Madrid yenye pointi moja zaidi, baada ya leo kuifunga Athletic Club 2-1. Real Madrid yenye pointi 70 za mechi 30, muda huu inamenyana na Rayo Valecano ikiwa tayari inaongoza kwa bao la Cristiano Ronaldo dakika ya 15, pasi ya Gareth Bale. 

  Wimbi la ushindi: Lionel Messi akishangilia baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa Barcelona wa 1-0 dhidi ya jirani zao Espanyol
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AIPAISHA BARCA LA LIGA, REAL YAJIKONGOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top