• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 26, 2014

  MESSI SASA KULIPWA ZAIDI YA RONALDO...HAYO NI MATUSI YA RAIS MPYA BARCA

  KLABU ya Barcelona itamfanya Lionel Messi kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani, kwa kumpa mshindi huyo wa Ballon d'Or nne mshahara wa zaidi ya Pauni 335,000 kwa wiki.
  Hiyo ni ahadi ya rais wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu inayokuja siku mbili tu baada ya nyota huyo wa Argentina kupiga hat-trick Barca ikiifunga Real Madrid na kurejea kwenye mbio za ubingwa.
  "Wote tunataka Messi awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani na hilo ndilo tunalolifanyia kazi kwa sasa,"alisema Bartomeu. "Hadi sasa tunaelekeza fikra zetu kwenye mashindano tunayoshiriki, lakini itatokea karibuni,".

  Neema inakuja: Lionel Messi akiwa mazoezini na wachezaji wenzake wa Barcelona jana mchana

  "Hakuna hapa anayetaka Messi auzwe. Huwezi kumuuza Leo. Alikuja hapa akiwa ana umri wa miaka 13 na ni mmoja wa wachezaji wetu.'
  Barcelona ilitoa ofa ya kwanza kwa baba yake Messi ambaye pia ni wakala wake, Jorge, mapema mwaka huu na inafahamika ofa hiyo imefanyia marekebisho pia kipengele cha klabu kumiliki asilimia 100 ya haki ya matumizi ya picha ya mchezaji huyo, ambayo ilikuwa haimpendezi mfungaji huyo wa kihistoria wa timu hiyo.
  Blow: Ronaldo (right) would become the second highest-paid player on the planet
  Anashuka: Ronaldo (kulia) atakuwa mchezaji wa pili kwa kulipwa zaidi Messi atakapoongezewa mshahara Barcelona 

  Rais huyo mpya anakabiliwa na presha ya kuwaridhisha mashabiki kwa kufanya wanachokipenda katika miezi yake sita ya mwanzo na jambo kubwa ni suala la Messi, ambaye Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2018. 
  Dili hilo linatarajiwa kujadili wakati Jorge Messi atakapoketi chini na Bartomeu kabla ya fainali ya Kombe la Mfalme Aprili 16, na kuongeza mwaka mmoja katikamkataba wa mchezaji huyo ili umalizike 2019 na atampiku Cristiano Ronaldo kwa mshahara akilipwa Pauni Milioni 17.5 kwa mwaka, ambazo ni sawa na Pauni 336,000 kwa wiki.
  Pamoja na kumuongezea mshahara ampiku Ronaldo, pia Barca itamruhusu Messi amiliki haki ya matumizi ya picha yake kwa asilimia 100.  Ronaldo kwa sasa anaingiza zaidi ya Messi, lakini Real Madrid inamiliki asilimia 50 ya haki za matumizi ya picha yake
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI SASA KULIPWA ZAIDI YA RONALDO...HAYO NI MATUSI YA RAIS MPYA BARCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top