• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 26, 2014

  MAN CITY YAIPIGA MAN UNITED 3-0, ARSENAL YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA SWANSEA

  KLABU ya Manchester City imewaangusha wapinzani wao Manchester United kwa mabao 3-0 usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford. 
  Mabao ya Man City usiku huu yamefungwa na mshambuliaji Edin Dzeko mawili dakika za kwanza na 26, pasi kutoka Samir Nasri na Yaya Toure dakika ya 90.
  Kiboko yao; Edin Dzeko amefunga mabao mawili Manchester City ikiilaza 3-0 Man United usiku huu

  Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo usiku huu, Arsenal imetoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Swansea City Uwanja wa Emirates, London.
  Mabao ya wenyeji yamefungwa Wilifried Bony dakika ya 11 na Matheu Flamini aliyejifunga dakika ya 90, wakati ya Arsenal yamefungwa na Lukas Podolski dakika ya 73 na Olivier Giroud dakika ya 74.
  Kipa Michel Vorm akipangua mpira juu ya mchezaji mwenzake, Nail Taylor na wachezaji wa Arsenal, Olivier Giroud na Tomas Risicky kulia 

  Nayo Newcastle United imefungwa nyumbani mabao 3-0 na Everton, mabao ya washindi yakifungwa na Barkley dakika ya 22, Lukaku 52 na Osman 88.
  Ushindi huo unaifanya City itimize 66 baada ya kucheza mechi 29 na kupanda hadi nafasi ya tatu, nyuma ya Liverpool yenye pointi 65 za mechi 30 wakati Chelsea yenye pointi 69 za mechi 31 inaendelea kujinafasi kileleni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIPIGA MAN UNITED 3-0, ARSENAL YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA SWANSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top