• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 26, 2014

  BAYERN MUNICH WATWAA UBINGWA UJERUMANI MAPEMAAA, TENA KWA REKODI YA KUSISIMUA

  KLABU ya Bayern Munich imetwaa taji la Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga kwa kuweka rekodi baada ya kuifunga Hertha Berlin mabao 3-1 usiku huu mjini Berlin.
  Shukrani kwao, Toni Kroos, Mario Goetze na Franck Ribery waliofunga mabao hayo na kuwapa ubingwa huo Bayern zikiwa zimebaki mechi saba ligi kumalizika.
  Mabingwa tena; Bayern Munich wamejihakikishia ubingwa wa Ujerumani kwa rekodi hya kusisimua usiku huu

  Washindi hao wa mataji matatu msimu uliopita, wamenyakua taji lao la 23 la Bundesliga tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 1963 kwa rekodi ya kushinda mechi 10 mfululizo.
  Hiyo inafanya Bayern Munich inayofundishwa na kocha Pep Guardiola ifikishe mechi 19 jumla za kushinda mfululilizo katika mashindano yoet na mechi 52 za ligi kucheza bila kufungwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BAYERN MUNICH WATWAA UBINGWA UJERUMANI MAPEMAAA, TENA KWA REKODI YA KUSISIMUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top