• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 31, 2014

  SUNGURA MJANJA WA MASHAUZI AACHIA MPYA

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam 
  MWIMBAJI chipukizi wa Taarab anayeinukia vizuri nchini, Saida Ramadhani ‘Sungura Mjanja’ ameibuka na wimbo mpya uitwao Ropokeni Yanayowahusu.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii katika hoteli ya Double Tree, Masaki, Dar es Salaam, mwimbaji huyo wa kundi la Mashauzi amesema kwamba wimbo huo ametungiwa na dada yake, Isha Ramadhani.
  Saida Ramadhani 'Sungura Mjanja' ana kitu kipya

  “Dada Isha katunga, mimi nimerekodi na umekwishakamilika, ni wimbo mzuri sana, naamini utapendwa ukitoka. Na utazidi kunipandisha matawi ya juu,”alisema Saida.
  Saida ameingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Kili mwaka huu kupitia wimbo wa Asiyekujua Hakuthamini, ambao ameshirikiana na dada yake, Isha ulioingia kwenye kipengele cha wimbo bora wa Taarab.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUNGURA MJANJA WA MASHAUZI AACHIA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top