• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 29, 2014

  DAVID SILVA FITI KUIVAA ARSENAL LEO, AGUERO BADO GONJWA

  KIUNGO David Silva anarejea kukiongezea nguvu kikosi cha Manchester City katika mchezo wa leo dhidi ya Arsenal Ligi Kuu ya England.
  Kulikuwa kuna wasiwasi Silva ataikosa safari ya Emirates baada ya kughairi kufanyiwa matibabu ya kifundo cha mguu alichoumia katika mchezo dhidi ya mahasimu, Manchester United Jumanne.
  Lakini kocha Manuel Pellegrini amethibitisha kwamba mchezaji wake huyo muhimu atakuwepo, ingawa mshambuliaji Sergio Aguero na beki Matija Nastasic wataendelea kuwa nje.
  Huduma za Silva: Kiungo wa kimataifa wa Hispania amekuwa mchezaji muhimu kikosini Manchester City
  Ruled out: Aguero chats to Pellegrini during training at Carrington on Thursday
  Atakuwa nje: Aguero akizungumza na Pellegrini wakati wa mazoezi huko Carrington Alhamisi

   "Ndiyo Silva yuko sawa, yumo kwenye orodha ya kikosi,"alisema Pellegrini katika Mkutano na Waandishi wa Habari. 
   "Timu hii hakika itakuwa sawa sawa na ileya wiki iliyopita huku Aguero na Nastasic wakiwa nje. Wachezaji wote wengine wapo fiti. Aguero anahitaji wiki moja zaidi.  Tutaona anaendeleaje wiki ijayo,"alisema.
   Ushindi kwa City utaiondoa Arsenal kwenye mbio za ubingwa na timu ya Pellegrini itaiacha kwa pointi 12 The Gunners ikiwa watashinda na mechi zao mbili za viporo.
   • Blogger Comments
   • Facebook Comments

   0 maoni:

   Item Reviewed: DAVID SILVA FITI KUIVAA ARSENAL LEO, AGUERO BADO GONJWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
   Scroll to Top