• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 29, 2014

  ARSENAL YAIKATALIA MAN CITY...SARE 1-1

  KLABU ya Manchester City imeshindwa kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 Arsenal Uwanja wa Emirates, London

  Kufuatia Chelsea kufungwa 1-0 na Crystal Palace katikqa mchezo uliotangulia leo, kikosi cha Manuel Pellegrini ambacho bado viporo vya mei, ilikuwa ina nafasi ya kupanda kileleni kwa wastani wa mabao kama ingeifunga Gunners.
  Pamoja na hayo licha ya kupata bao la mapema lililofungwa na David Silva dakika ya 18, Arsenal iliawazisha kupitia kwa Mathieu Flamini dakika ya 53.
  Liverpool itakuwa mwenyeji wa Tottenham Jumapili na sasa ubingwa upo kwenye himaya yao, kwa kuwa City na Chelsea zitakwenda Anfield.
  Mkombozi: Mathieu Flamini akishangilia baada ya kuifungia bao la kusawazuisha ArsenalElation! David Silva roars with delight after putting Manchester City ahead in the first half
  La kuongoza! David Silva akishangilia baada ya kuifungia bao la kuongoza Manchester City
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAIKATALIA MAN CITY...SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top