• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 20, 2014

  WENGER KUPEWA TUZO YA KUPIGA KAZI MUDA MREFU ARSENAL KESHO, JUMAMOSO ATAIONGOZA TIMU KATIKA MECHI YA 1,000

  KLABU ya Arsenal itamkabidhi tuzo ya kufanya muda mrefu zaidi kocha wao, Arsene Wenger akielekea kutimiza mechi ya 1,000 tangu aanze kupiga mzigo The Gunners.
  Wenger, ambaye alianza kazi karika klabu hiyo Agosti mwaka 1996, atatimiza mechi hizo Jumamosi Uwanja wa Stamford Bridge na klabu hiyo itamkabidhi tuzo hiyo katika viwanja vya mazoezi, Colney mjini London kesho.
  Taarifa kamili kuhusu kukabidhi tuzo hiyo zinafanywa siri, lakini tuzo hiyo itakabidhiwa wakati wa mazoezi kwa kuwa Mfaransa huyo hajataka hilo lichanganywe katika siku ya mechi.
  Tuzo: Arsenal itampatia Arsene Wenger tuzo ya kufanya kazi muda mrefu akielekea kutimiza mechi ya 1,000 Jumamosi
  Day one: The Frenchman took charge of the club in August 1996
  Siku ya kwanza: Mfaransa huyo alichukua mikoba ya kuinoa Arsenal Agosti mwaka 1996

  Mwenyekiti wa Arsenal, Sir Chips Keswick na Mwenyekiti wa Chama cha Makocha wa Ligi Kuu, Richard Bevan wote watahudhuria.
  Katika miaka yake 18 ya kufanya kazi klabu hiyo ya London,Wenger ameshinda mechi 572, ametoa sare mechi 235 na kufungwa mechi 192 katika mechi 999 hadi sasa.
  Pamoja na hayo, Wenger hajawahi kuifunga Chelsea ikiwa na kocha Mreno, Jose Mourinho, hadi sasa akiwa amefungwa mechi tano, sare tano katika mechi 10 baina yao.
  Mourinho hajawahi kufungwa mechi nyumbani katika Ligi Kuu ya England akiwa kocha wa Chelsea, katika mechi 75 hadi sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WENGER KUPEWA TUZO YA KUPIGA KAZI MUDA MREFU ARSENAL KESHO, JUMAMOSO ATAIONGOZA TIMU KATIKA MECHI YA 1,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top