• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 21, 2014

  PONDAMALI WA ENYIMBA ATUPIWA VIRAGO, KISA KUMLAZIMISHA KIPA KUDAKA NA TIMU IKAFUNGWA NYUMBANI

  Na Princess Asia, Dar es Salaam
  MABINGWA mara sita wa Ligi Kuu ya Nigeria iitwayo NPFL, Enyimba wametangaza kumfukuza kazi kocha wao wa makipa, Shuaibu Suleiman.
  Suleiman alisimamishwa Machi 2, mwaka huu mara tu baada ya Enyimba kufungwa nyumbani mabao 2-1 na AS Real Bamako ya Mali katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Alisimamishwa kwa kumpendekeza kipa Femi Thomas acheze mechi hiyo wakati alikuwa hajisikii kucheza.
  Mwenzake katimuliwa Enyimba; Kocha wa makipa wa Yanga SC, Juma Pondamali kulia akizungumza na kipa wa timu hiyo, Juma Kaseja juzi wakati wa mapumziko katika mchezo baina ya timu hiyo na Azam FC uliokwisha kwa sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

  Mwenyekiti wa Enyimba, Chief Felix Anyansi-Agwu amesema kwamba Suleiman hatarudishwa kutoka kwenye adhabu.
  Thomas hajadaka tena Enyimba tangu kipigo cha AS Real Bamako, lakini Anyansi amesema wanamuheshimu sana kipa huyo wa zamani wa Ocean Boys.
  “Femi Thomas ni mmoja kati ya makipa bora Nigeria. Kila mmoja aliona alichokifanya msimu uliopita na hajawahi kuwa kipa mbaya. Tunafurahia kuwa naye hapa,”alisema.
  Enyimba imeshinda mechi mbili na sare moja katika mechi zake tatu tangu ifungwe na AS Real Bamako mjini Aba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PONDAMALI WA ENYIMBA ATUPIWA VIRAGO, KISA KUMLAZIMISHA KIPA KUDAKA NA TIMU IKAFUNGWA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top