• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 25, 2014

  MAHAKAMA YAAGIZA TFF IIKATE YANGA SC MILIONI 106 KUWALIPA WACHEZAJI

  Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) kukamata Sh. Milioni 106 za klabu ya Yanga kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake, Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.
  Taarifa ya TFF imesema kwamba, tayari wameanza utekelezaji wa amri hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa Machi 22 mwaka huu mjini Tabora walizuia Sh. 9,221,250 ambazo ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika mchezo huo ulioingiza jumla ya sh. 38,655,000.
  Wisdom Ndhlovu wa pili kulia waliosimama katika kikosi cha Yanga SC mwaka 2009

  Wachezaji hao walifungua kesi kortini kupinga mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa haki zao za kimkataba. Malashi na Ndlovu walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo ya sh. milioni 106.
  Tunawakumbusha wanachama wetu (klabu za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na vyama shiriki) kuzingatia mikataba wanayoingia na watendaji wao wakiwemo wachezaji, makocha na maofisa wengine.
  “Iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka kufanya hivyo,”imesema taarifa ya TFF.
  Wisdom Ndhlovu kulia akiwa na Stephen Malashi kushoto, hapa walikuwa kwenye ndondo wakiicheza Golden Bush FC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAHAKAMA YAAGIZA TFF IIKATE YANGA SC MILIONI 106 KUWALIPA WACHEZAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top